Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TFF: JPM alitusaidia kuaminiwa na Fifa

8d5d1242468c0d7ccc415255cc5f142d.png TFF: JPM alitusaidia kuaminiwa na Fifa

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema litamuenzi Rais John Magufuli kwa kudumisha nidhamu kwenye matumizi ya fedha.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa TFF jana Kidao Wilfred alipozungumza na gazeti hili kuhusu kifo Rais Magufuli kilichotokea Jumatano ya wiki hii kutokana na maradhi ya moyo.

Kidao alisema Rais Magufuli alikuwa mwana michezo kwa vitendo kwani muda wote alikuwa anashuhudia mechi za timu ya Taifa na kutoa hamasa na alipotoa fedha alisisitiza zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Rais Magufuli alikuwa mwanamichezo kwa vitendo kwani muda wote alikuwa anashuhudia mechi za timu ya Taifa na kutoa hamasa na ile kauli yake ya ‘pesa hizi zikatumike kwa malengo yaliyokusudiwa vinginevyo mtazitapika’ tuliipokea vizuri kwa sababu tumekuwa tukiishi kwa nidhamu kwenye matumizi ya fedha,” alisema Kidao.

Alisema nidhamu ya fedha ambayo Rais Magufuli alikuwa akisisitiza iliwasaidia kwani ndiyo maana FIFA wamekuwa na imani kubwa na TFF na kuwapa miradi miwili mikubwa ambayo walitamani Magufuli angeishuhudia ikikamilika.

“Nidhamu ya fedha ilitusaidia ndiyo maana FIFA wamekuwa na imani kubwa na sisi na kutupatia miradi miwili mikubwa ambayo tulitamani angeshuhudia wakati inakamilika lakini ndio hivyo kazi ya Mungu haina makosa,” aliongeza.

Miradi anayozungumzia Kidao ni ule wa Tanga utakaokuwa na uwanja na hosteli na ule wa Kigamboni. Pia Kidao alisema Rais Magufuli atakumbukwa kwa hotuba yake ya mwisho akizindua Bunge mwishoni mwa mwaka jana baada ya uchaguzi kuhusu uwekezaji mkubwa katika michezo.

“Tutamuenzi kwa kuhakikisha tunasimamia vizuri rasilimali za mpira wa miguu na kusimamia vizuri shughuli zote za mpira wa miguu na kuongeza ajira kama alivyoamini katika kutengeneza viwanda ili kuongeza ajira.

Chanzo: www.habarileo.co.tz