Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TANZIA: Msanii wa sarakazi afariki akifanya mazoezi

Msanii Sarakasi.jpeg Marehemu Frank Idd Mwaluka

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Menejimenti na Wafanyakazi wa BASATA wanatoa pole kwa familia na Wasanii kufuatia kifo cha Msanii wa mchezo wa Sarakasi nchini Tanzania,Marehemu Frank Idd Mwaluka kilichotokea tarehe 09 Sept. 2023 katika mji wa Istanbul nchini Uturuki.

Taarifa kutoka kwa kaka wa Marehemu Bw. William Idd Mwaluka zinasema kifo cha Marehemu Frank Idd Mwaluka kilitokana na kudondoka kutoka juu wakati wakifanya mazoezi na wenzake.

Aidha Bw. William amesema kuwa, kwa hivi Sasa msiba upo maeneo ya Ubungo nyuma ya kanisa la Mchungaji Gwejima.

Marehemu Frank Idd Mwaluka alisajiliwa BASATA kwa usajili: BST-9684-2023-213 na aliondoka nchini tarehe 30 /05/2023 kuelekea Uturuki kikazi akiwa na Kikundi cha Sarakasi (TES) na alitarajia kurekejea nchini Tanzania tarehe 25/11/2023.

Pumzika kwa Amani mpendwa wetu Frank Idd Mwaluka. Daima tutakukumbuka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live