Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sven asema kazi ipo msimu ujao

5b8ebb6357a8fbbff1fa61a01056b1dc Sven asema kazi ipo msimu ujao

Mon, 24 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KOCHA wa Simba, Sven Vandebroeck amesema amefurahishwa na ubora wa kikosi alichonacho ila anaona msimu ujao utakuwa mgumu katika kuchagua wachezaji wa kikosi cha kwanza.

Vandebroeck aliyasema hayo juzi Dar as Salaam baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Vital O ya Burundi katika kuadhimisha wiki ya ya Simba iliyohitimishwa kwenye Uwanja wa Mkapa na kuhudhuriwa na maelfu ya mashabiki wake.

Alisema asilimia kubwa ya wachezaji walionesha juhudi kubwa na kuwa wana nguvu ila kuna baadhi ya vitu vichache vinavyotakiwa kurekebishwa ili kufanya mabadiliko na kufanya vizuri zaidi msimu ujao.

“Wengi wana nguvu na wameonesha juhudi ni baadhi tu ya vitu vichache vinahitaji kurekebishwa kuweka mambo sawa, kunahitaji muunganiko mzuri katika safu ya ulinzi, viungo na ushambuliaji, hivyo kwa wiki moja iliyobaki tutaweka mambo sawa,” alisema.

Kocha huyo wa mabingwa alisema anafikiri msimu ujao utakuwa mgumu zaidi katika uchaguzi wa wachezaji na kuwataka wachezaji wake kuendelea kubaki katika ubora, huku akiwahimiza wale watakaokosa nafasi kikosi cha kwanza wasikate tamaa bali kujitahidi zaidi na kukubali hali itakayotokea.

“Najua haitakuwa rahisi kila mmoja kucheza, wapo watakaoanzia benchi na wengine wataaza, hawatakiwi kukata tamaa na siku zote sikubaliani na wanaokata tamaa bali kukubali hali hiyo ila kuhakikisha wanakuwa katika ubora wakati wote,” alisema.

Alisema kwa sasa wanawaza mchezo wao ujao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Namungo utakaochezwa Jumapili Arusha hivyo wana muda mchache wa kufanya maandalizi huku akitaja wachezaji wawili Luis na Paschal Wawa kuwa wataendelea kukosekana akisema walioko majeruhi kama Francis Kahata na Erasto Nyoni anaamini watakuwa wameimarika.

Alisema mchezo ujao huenda ukawa mgumu kwani Namungo sio kama Vital O wanaonekana wepesi, bali ni wagumu na hivyo wanatarajiwa kuanza safari yao ya Arusha Ijumaa ijayo.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu walitumia wiki ya Simba kutambulisha wachezaji wao watakaokuwepo msimu ujao ikiwa imebaki siku chache kuanza kwa michuano hiyo Septemba 6, mwaka huu.

Chanzo: habarileo.co.tz