Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sven afunguka usajili Simba SC

89764 Sven+pic Sven afunguka usajili Simba SC

Tue, 24 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Simba Sven Vandenbroeck, amesema anataka mshambuliaji asilia katika dirisha dogo la usajili.

Sven ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuiongoza Simba kupata ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya AFC Arusha katika mchezo wa Kombe la FA kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, juzi.

Hii ni mara ya kwanza kocha huyo kuzungumzia usajili tangu alipotwaa mikoba ya Patrick Aussems ambaye mkataba wake ulisitishwa.

Tayari Simba imeanza mchakato wa kumsajili winga wa UD Songo, Luis Jose ambaye pia ana uwezo kucheza nafasi ya mshambuliaji.

Akizungumza jana, Sven alisema ameona wachezaji 19 tangu alipoanza kazi na amebaini ubora na kasoro zao.

Sven alidokeza amevutiwa na kiwango cha Meddie Kagere, lakini John Bocco na Wilker Da Silva hawako imara kwa ushindani, hivyo anahitaji kuongeza nguvu katika eneo hilo.

Wakati Kagere amefunga mabao manane, Bocco na Da Silva wamekosa mechi za msimu huu kutokana na majeruhi. Kagere anafuatiwa na winga Miraji Athumani aliyefunga mabao saba.

Pia alisema amebaini kasoro ndogo katika mchezo dhidi ya AFC Arusha ambapo wachezaji wake walishindwa kuanza kucheza kuanzia nyuma jambo ambalo atalifanyia kazi.

“Kipimo ambacho nitatumia kuona uwezo wa kila mchezaji kabla sijafanya uamuzi ni mechi nne ambazo tutacheza na mazoezi ambayo tunaendelea, lakini lazima nipate mshambuliaji mmoja,” alisema Sven.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa alisema sven amepewa jukumu la kusajili aina ya mchezaji anayemtaka na uongozi utamuunga mkono.

Senzo alisema endapo Sven anataka mshambuliaji watakuwa jukumu la kupendekeza mchezaji anayemtaka katika kuboresha kikosi chake.

Chanzo: mwananchi.co.tz