Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sven, Mugalu wanogesha Simba

Aada0f7e2acdb4e002b69b7fd6e101b3.jpeg Sven, Mugalu wanogesha Simba

Mon, 17 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU ya Simba imemsajili mshambuliaji wa kimataifa kutoka DR Congo, Chris Mugalu ‘Killer bull’, kutoka klabu ya Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka miwili.

Kabla ya kumtambulisha mchezaji huyo ambaye anafanya Simba kufikisha wachezaji 13 wa kimataifa, kuna tetesi za kuachwa wachezaji watatu,walianza kwa kumtambulisha beki, Ibrahim Ame kutoka Coastal Union kama mchezaji huru kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mugalu anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa kutoka Dynamos baada ya juzi Simba kumtambulisha kiungo, Larry Bwalya ‘Locomotive’ na anakuwa mchezaji wa nne wa kimataifa baada ya kiungo Bernard Morrison na beki Joash Onyango kumwaga wino kwa ajili ya msimu ujao.

Nyota huyo anaungana na washambuliaji wawili tegemeo wa Simba, John Bocco na Meddie Kagere, kuimarisha safu ya ushambuliaji.

Kagere alifunga mabao 22 na Bocco alifunga mabao 9 kati ya 78 yaliyofungwa na Simba ambayo imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo nguvu ya ushambuliaji inaongezeka kwa mabingwa hao wa ligi mara tatu mfululizo.

Mugalu ambaye amecheza misimu minnePower Dynamos, msimu wa 2017 ilifunga mabao 21 na kutwaa kiatu cha ufungaji bora.

Pia Simba imemsajili beki David Kameta kutoka Lipuli FC na Charles Ilamfya kutoka KMC.

Tetesi zinaeleza kuwa, Simba itaachana na Deo Kanda baada ya TP Mazembe ambayo ndio wamiliki wa mchezaji huyo kutaka wapewe dola za Marekani 50,000 ili asaini mkataba mpya lakani wakakataa, wengine ni beki Tairone Santos na kiungo Sharaf Shiboub ambaye mkataba wake umemalizika.

Kikosi cha Simba ni, makipa Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ali Salim, mabeki wa kushoto ni Shomari Kapombe, David Kameta, beki wa kulia ni Mohamed Husein, na mabeki wa kati ni Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Joash Onyango, Kenedy Juma, Ibrahim Amen a Yusuf Mlipili.

Viungo ni Jonas Mkude, Gerson Fraga, Mzamiru Yassin na Said Ndemla, viungo washambuliaji ni Clatous Chama, Hassan Dilunga, Francis Kahata, Luis Maquissoine, Shiza Kichuya na Juma Rashid.

Wengine ni Ibrahim Ajib, Miraji Athuman, Bernard Morrison na Larry Bwalya na washambuliaji ni Meddie Kagere, John Bocco, Charles Ilamfya na Chris Mugalu.

Pia kocha Sven Vandenbroeck amerejea nchini jana kuanza maandalizi ya mchezo wa ngao ya jamii unaotarajiwa kuchezwa Agosti 29 baada ya kuondoka

ligi ilipomalizika.

Wakati huohuo, Namungo jana ilimtambulisha beki Jafari Mohamed kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Yanga.

Chanzo: habarileo.co.tz