Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sure boy amalizana na Yanga

5f7f932a2a267794de495ac3537521aa.jpeg Sure boy amalizana na Yanga

Thu, 23 Dec 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KIUNGO Salum Abubakari ‘Sure boy’ amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga baada ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Azam FC.

Mkataba wa mchezaji huyo na Azam FC ulikuwa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji huyo aliwasilisha barua katika klabu yake ya Azam FC kuomba kuvunja mkataba kwa timu hiyo aliyoitumikia tangu mwaka 2007.

Msemaji wa Azam FC Zakaria Thabiti aliliambia gazeti hili Dar es Salaam jana kuwa Bodi ya klabu hiyo imemkubalia mchezaji huyo kuondoka na kwenda kokote anakotaka baada ya kumalizana naye kwa kuvunja mkataba huo.

“Sure boy ni mchezaji wetu, tulisikia kwamba ameleta barua kuomba kuvunja mkataba na bodi imemkubalia kwa hiyo anaweza kwenda popote anapotaka,” alisema Thabit.

Chaguo la mchezaji huyo kwa muda mrefu lilitajwa kuwa ni Yanga na msimu uliopita ilibaki kidogo tu asaini katika timu hiyo ya mitaa ya Twiga na Jangwani ila ilishindikana baada ya Azam kuwahi kumpa mkataba mpya.

Meneja wa mchezaji huyo Heri Mzozo alisema tayari mteja wake huyo amesaini Yanga miaka miwili.

“Nathibitisha kuwa ‘Sure boy’ amesaini mkataba wa miaka miwili Yanga baada tu ya kumalizana na uongozi wa Azam FC kwa hiyo sasa hivi ni mchezaji halali wa Yanga,” alisema.

Abubakari na wenzake Aggrey Moris na Mudathir Yahaya awali walisimamishwa na Azam FC kutokana na tatizo na utovu wa nidhamu ambapo wiki iliyopita waliitwa kurudi klabuni kuendelea na majukumu yao na yeye alikataa kurudi akitaka kuvunja mkataba ila wenzake walirudishwa kundini baada ya kuomba msamaha.

Chanzo: www.habarileo.co.tz