Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stephen Curry kufanyiwa vipimo vya MRI scan 

5282 4A8116BB00000578 5539169 The Warriors Star Looked In Distress After Hobbling Off During T A 10 TZW

Sun, 25 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mchezaji mpira wa kikapu raia wa Marekani, Stephen Curry hapo jana amejikuta akishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu wa kulia wakati walipokuwa wakiikabili timu ya Atlanta Hawks.



Curry anayekipiga ndani ya klabu ya Golden State Warriors amepata majeraha hayo wakati akiwa ndiyo anarejea baada ya kuikosa michezo sita kufuatia kusumbuliwa na majeraha ya goti lake la kushoto.

Katika mchezo huo Curry ameshinda jumla ya pointi 29 kabla ya kutolewa nje kufuatia kuumia na hivyo mchezo huo kumalizika kwa timu ya Atlanta Hawks kuibuka na ushindi wa jumla ya vikapu 106-94.

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Warriors inasema kuwa mchezaji huyo anatarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo vya MRI siku ya Jumamosi.

Chanzo: bongo5.com