Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yawanyima fursa Fei, Makame, Mnata kukutana na Wanayanga

69823 Tars+pic

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

WAKATI Yanga inasherehekea kilele cha Wiki ya Mwananchi leo Jumapili ambapo watatambulisha wachezaji wao ambao watawatumia msimu ujao, wapo nyota ambao watakosekana kwenye tukio hilo kutokana na jukumu walilonalo la kitaifa.

Wachezaji hao Fei Toto, Paul Godfrey, Kelvin Yondan, Metacha Manata na Abdul Aziz Makame wapo na timu ya taifa Stars ambayo leo pia inacheza mchezo wao wa marudiano wa kufuzu fainali za Chan kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani dhidi ya Kenya.

Mbali na wachezaji hao Meneja wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' naye hatashiriki tukio hilo kwani yupo nchini Kenya na Stars.

Wachezaji wawili ndio wageni machoni mwa wanachama wa Yanga ambao ni Makame na Mnata  waliosajili msimu huu, hivyo  mashabiki  wao watawasubiri kuwaona mpaka ligi kuu Bara ama michuano ya kimataifa itakapoanza.

Lakini Yondan, Fei Toto na Paul Godfrey sio wageni na mashabiki wa Yanga na tayari uwezo wao unajulikana, kikubwa kinachosubiriwa kwao ni ushindani.

Cannavaro amesema anaamini Yanga msimu ujao itakuwa na ushindani wa hali ya juu, akidai imesajili kikosi kipana ambacho kinatambulishwa mbele ya wanachama.

"Ni kitu kizuri na mashabiki watawajua wachezaji ambao watakabidhiwa malengo ya klabu kwa msimu unaotarajia kuanza msimu huu,"anasema.

Chanzo: mwananchi.co.tz