Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yafanya kweli

6ec810e86873e036a69461e77acd2929.jpeg Stars yafanya kweli

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TIMU ya Taifa ya soka, Taifa Stars, imewapa raha mashabiki baada ya kuifunga Madagascar kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia, Qatar 2022 uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam jana.

Katika mchezo huo ambao ulichezwa bila mashabiki, Taifa Stars ilipata bao la kuongoza kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Erasto Nyoni baada ya Simon Msuva kufanyiwa faulo eneo la hatari.

Baada ya bao hilo Taifa Stars ilitawala mchezo kwa dakika 20 lakini pia ilipoteza nafasi mbili za kufunga mabao kupitia kwa Feisal Salum na Mbwana Samatta.

Dakika ya 26, Novatus Dismas alifunga bao la pili baada ya kuwalamba chenga walinzi wa Madagascar na kuachia shuti lililomshinda kipa Adrian Melvin wa Madagascar.

Madagascar walipata bao la kwanza likifungwa na Njiva Rokotomarimalala aliyeingia dakika ya 31 kuchukua nafasi ya Manampisoa Lalaina na Fontein Thomas alisawazisha na matokeo kuwa 2-2 na kwenda mapumziko wakiwa nguvu sawa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na dakika ya 53 Feisal alifunga bao la tatu akiunganisha pasi ya Samatta na baada ya bao hilo kocha Kim Poulsen alifanya mabadiliko kadhaa.

Kim aliwatoa Reliant Lusajo na Novatus Dismas na kuwaingiza Nickson Kibabaje na Mudathir Yahya na baadaye alimtoa Feisal na kuingia Salum Abubakar.

Kwa matokeo hayo Taifa Stars inaongoza Kundi J ikiwa na pointi nne sawa na Benin zikitofautiana kwa kwa uwiano wa mabao, DRC ikishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi moja na Madagascar haina pointi.

Wakati huo huo, Ethiopia imepanda hadi nafasi ya pili katika Kundi G baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe mjini Bahir Dar.

Kwa matokeo hayo Ethiopia na Ghana zina pointi tatu, Zimbabwe inashika mkia ikiwa na pointi moja na vinara ni Afrika Kusini ikiwa na pointi nne.

Chanzo: www.habarileo.co.tz