Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars ya Ufukweni,Uganda vitani leo

Ufukwen Ed Stars ya Ufukweni,Uganda vitani leo

Mon, 24 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Akizungumza na gazeti hili jijini jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Boniface Pawassa, alisema wamewasili nchini Senegal na kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Uganda.

Alisema wamejiandaa vizuri na wamepata nafasi ya kuwasoma wapinzani wao Uganda katika mechi ya kwanza waliyocheza na Senegal jana kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo.

"Tumepata nafasi ya kuwaona wapinzani wetu, tumepata tathimini ya jinsi wanavyocheza, naamini ni tathmini nzuri kwa mechi yetu katika kuhakikisha tunaenda kufanya vizuri katika mechi yetu ya kwanza," alisema Pawassa.

Tanzania imepangwa Kundi A ya michuano hiyo pamoja na Uganda na wenyeji wa mashindano hayo, Senegal ambao wataikaribisha Tanzania Mei 26, mwaka huu.

Chanzo: ippmedia.com