Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stand United yaivizia Simba

44115 Pic+stand Stand United yaivizia Simba

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

STAND United watawakaribisha Simba Jumapili ya wiki hii, lakini Kocha wake Athumani Bilali ‘Bilo’ amesema hawaachi kitu msimu huu na kilichowatokea Yanga ndicho kitakachowakuta Wekundu hao wa Msimbazi.

Tayari Stand United imeondoka mjini Shinyanga na kwenda kujichimbia katika kijiji cha Isaka kilichopo wilayani Kahama kwa ajili ya kujiwinda na mchezo huo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Bilo alisema anajua ugumu wa mchezo huo lakini msimu huu wamejipanga kuhakikisha timu hizo mbili kubwa hazichomoki Shinyanga.

“Nilisema tutawafunga Yanga wengi wakadhani naongea tu kujifurahisha lakini sasa nasema Simba tutawakalisha najua mechi itakuwa ngumu lakini hilo halitumizi kichwa kabisa,”alisema Bilo.

Alisema kwa sasa wapo katika mazoezi makali kujiwinda na mchezo huo ambao amesema aliwaangalia Simba juzi kwenye mchezo wao na Lipuli ambapo amejua namna ya kuweza kuwathibiti Wekundu hao.

“Tupo hapa Isaka tumeweka kambi tunajifua kikubwa tushajua pa kuwathibiti Simba wasifanye lolote kwenye mchezo wa jumapili nihaidi tu lazima ushindi upatikane ,”alisema Kocha huyo.

Hata hivyo, Kocha huyo alisema amepata faraja kuona mpaka sasa hakuna mchezaji  mwenye majeruhi ambao ataukosa mchezo huo wa Jumapili ambapo amesema nyota wake wote wako fiti.



Chanzo: mwananchi.co.tz