Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Staa wa Bongo fleva, awabebesha mzigo Kagere, Okwi na Bocco

47037 Pic+bocco

Mon, 18 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Msanii chipukizi wa Bongo Fleva anayejulikana kwa jina maarufu Bright, amewataka Meddie Kagere, Emmanuel Okwi kuwaamisha Watanzania uwepo wao ndani ya timu hiyo kama wachezaji wa kigeni, huku akimsisitiza John Bocco kuibeba nchi mabegani mwake dhidi ya As Vita.

Bright amesema kile anachokifanya Okwi na Kagere kwenye ligi kuu Bara, wakidhihirishe dhidi ya As Vita, huku Bocco akimtaka awe mstari wa mbele kuzifumania nyavu ili aweke rekodi ya kukumbukwa kwa siku za mbele.

"Bocco ndiye mzawa ambaye atakuwa safu ya ushambuliaji, anatakiwa kuonyesha uchungu zaidi wa kuhakikisha Simba inashinda, ikishinda watakuwa wameliwakilisha taifa kwa sifa njema dhidi ya wengine.

Bright aliyewahi kutamba na nyimbo mbalimbali za bongo fleva ikiwemo na Nitunzie, hakuficha mapenzi yake dhidi ya Simba na kudai alikuwa anamkubali Shiza Kichuya ambaye kwa sasa anacheza ENPPI ya Misri.

 "Kichuya alikuwa na roho ya kujituma, sina maana kwamba waliopo hawajitumi na siwapendi la,"anasema.



Chanzo: mwananchi.co.tz