Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Sports Countdown' ya EA Radio leo Agosti 17

Courtis 'Sports Countdown' ya EA Radio leo Agosti 17

Tue, 17 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

'Sports Countdown' ya leo Agosti 17, 2021 inakukaribisha wewe mdau wa michezo kuzihesabu zile stori sita kali za kimichezo na kila siku saa moja na robo kwenye 'Supa Breakfast' ya East Africa Radio 88.1 DSM.

6 - Ni idadi ya wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha hili kubwa la usajili na mabingwa wa kihistoria wa kombe la Shirikisho nchini la 'TFF ASFC', Klabu ya Simba huku idadi hiyo ikifikia Sita baada ya usiku wa jana kuthibitisha kumsajili mlinzi wa kulia na nahodha wa mabingwa wa CECAFA U23 - Tanzania U23, Israel Patrick Mwenda kwa kandarasi ya miaka miwili kutoka klabu ya KMC.

Mwenda anafanya idadi ya wachezaji wazawa waliosajiliwa na Simba mpaka sasa kuwa wawili baada ya Yusuph Mhilu kutoka Kagera Sukari. Wengine waliosajiliwa ni Peter Banda, Duncan Nyoni, Pape Ousmane Sakho na Henock Inonga Baka.

5 - Ni idadi ya miaka iliyopita tokea mcheza tennis Deniil Medvedev raia wa Urusi mwenye miaka 25 arekodi ushindi wake wa kwanza wa mchezo huo kwenye mashindano ya Ricoh Open yaliyofanyika nchini Uholanzi mwaka 2016.

Medvedev ambaye anashikilia nafasi ya pili kwenye viwango vya ubora vya mchezo wa tenisi Duniani kwa upande wa wanaume, ameendelea kuwa na wakati mzuri baada ya hapo jana kumfunga Reilly Opelka raia wa Marekani kwa seti 6-4, 6-3 na kutwaa ubingwa wa Canadian Open 2021 mashindano yaliyofanyika Toronto nchini Canada ikiwa ni michezo ya  kujiweka sawa kabla ya US open inayotaraji kuanza Agosti 30 mwaka huu nchini Marekani.

Kwa upande wa wanawake, kombe hilo limeenda kwa Mwanadada Camila Giorgi raia wa Italy anayeshika nafasi ya 71 duniani baada ya kumchapa Karolina Pliskova wa Czech kwa seti 6-3, 7-5 na kurekodi taji lake la kwanza la mashindano hayo.

4 - Ni idadi ya wastani wa rebound alizopiga mcheza kikapu, Eric Bledsoe kwa msimu uliopita wa mwaka 2020-2021 akiwa na timu ya New Orleans Pelicans.

Mlinzi huyo mwenye miaka 31 amethibitishwa kujiunga na timu yake ya zamani ya Los Angeles Clippers kutoka klabu iliyokuwa inammiliki Memphis Glizzles na kufanya makubaliano ya mabadilishano ya wachezaji kama sehemu ya kumhamisha Bledsoe kwenda Glizzles. Wachezaji watatu waliotoka Clippers na kwenda Glizzles kama sehemu ya mabadilishano ya uhamisho wa Bledsoe kwenda Clippers, ni Patrick Beverley, Rajon Rondo na Daniel Oturu.

Bledsoe alikipiga Lakers kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2010-2013.

3 - Ni idadi ya miaka ambayo kipa wa sasa wa Real Madrid, Thibaut Courtis ameitumikia klabu hiyo tokea ajiunge nao akitokea Chelsea ya England msimu wa mwaka 2018 na hatimaye kufanikiwa kushinda mataji matatu, lile la La Liga, Spanish Super Cup na Kombe la dunia la vilabu.

Mkali huyo wa kuchomoa michomo awapo langoni ambaye pia usiku wa jana alifikisha michezo 100 akiwa na Real Madrid kwenye michezo ya ushindani, amefanikiwa kurefusha mkataba wake ambapo usiku wa kuamkia leo amesinya kandarasi ya miaka 5 kuendelea kusalia na mabingwa hao wakihistoria wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya hadi mwaka 2026.

2 - Ni idadi ya miaka aliyohudumu Dr. Jonas Tiboroha akiwa Khatibu Mkuu kwenye klabu ya Yanga kuanzia mwaka 2014 na kujiuzulu mwaka 2016 kabla ya kurejea tena klabuni hapo miaka mitatu baadaye mwaka 2019 na kugombea urais ambapo alishindwa kwenye uchaguzi mkuu kwa klabu hiyo.

Baada ya kuwa benchi kwa muda fulani, hatimaye 'waoka mikate' klabu ya Azam imemtangaza mkali huyo anayesifika kwa misimamo dhabiti katika kuliongoza soka kuwa mkurugenzi wao wa soka cheo ambacho hakikuwepo Azam hivyo uteuzi wake ni wakihistoria klabu hapo.

Baada ya kutangazwa Tiboroha amesema kazi yake kubwa ni kuchochea na kusimamia shughuli zote za maendeleo ya soka klabuni hapo.

1 - Ni idadi ya assist aliyotoa kiungo Granit Xhaka kwenye michezo minne aliyoichezea timu yake ya taifa ya Uswizi na kuisaidia kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya UEFA EUROS iliyomalizika mwezi uliopita.

Kiungo huyo ambaye ni hodari wa kupiga pasi za umbali mrefu na kufunga magoli kwa mashuti makali amepata bingo kwani usiku wa kuamkia leo ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja kuendelea kubakia na klabu yake ya Arsenal hadi mwaka 2024 na kuzima fununu na nyota huyo kutimkia AS Roma ya Italia.

Chanzo: eatv.tv