Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Sports Countdown' ya EA Radio leo Agosti 12

JOHANNA 1 'Sports Countdown' ya EA Radio leo Agosti 12

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

'Sports Countdown' ya EA radio inakupitisha kuhesabu zile stori kali sita za kimichezao zilizojiri, kubwa zaidi ni Lionel Messi kusajiliwa na kuthibitishwa rasmi kujiunga PSG na kusema ndoto yake kubwa ni kutaka kuendelea kushinda mataji hususani kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Submitted by George David on Alhamisi , 12th Aug , 2021 Mcheza tennisi anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora kwa upande wa wanawake,Johanna Konta akiwa kwenye moja ya mchezo kwenye michuano ya French Open mwaka huu.

6 - Ni idadi ya assist alizotoa winga Dickson Ambundo msimu uliopita akiwa na timu ya Dodoma Jiji pamoja na kufunga mabao 4 hivyo kuhusika kwenye mabao 10 kwenye VPL pekee na kuisaidia timu yake kushika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi kuu ilhali ukiwa ni msimu wake wa kwanza baada ya kupanda daraja na kucheza ligi hiyo mwaka 2020-2021.

Mkali huyo wa kumimina krosi hivi sasa ni mchezaji wa Yanga na hii ni baada ya usiku wa jana kuthibitishwa na kutambulishwa rasmi kujiunga na mabaingwa hao wakihistoria wa Ligi kuu nchini kwa kandarasi ya miaka miwili na kufanya orodha ya wachezaji wazawa waliosajiliwa na Yanga akiwemo Yusufu Athumani pamoja na David Bryson ambaye bado hajatangazwa.

Ambundo pia anafanya orodha ya wachezaji wapya wliosajiliwa na Yanga hivi sasa kufika saba ambao ni Fiaston Abdulrazack, Heritier Mkamabo, Djigui Diarra, Khaleed Haucho, Erick Johora, Yussufu Athumani na Dickson Ambundo.

5 – Ni idadi ya penalti walizofungwa na timu ya Liverpool ilipocheza dhidi ya Chelsea kwenye fainali ya UEFA SUPER CUP 2019 na kubeba ubingwa huo huku ikiiacha Chelsea walipata peanlti 5 kuondoka vichwa chini kwa kufungwa mara tatu mfululizo kwenye fainali hizo baada ya kufungwa naAtletico Madrid 2012 na klabu ya Bayern Mwaka 2013.

Chelsea imesafisha nyota baada ya kuifunga nyambizi wa Hispanua, timu ya Villareal kwa penalty 6-5 na kutwaa ubingwa wa UEFA super cup kwa mara ya kwanza tokea mwaka 1998 ilhali ukiwa ni ubingwa wao wa wapili kwenye historia ya fainali hiuzo. Shujaa wa mchezo huo alikuwa ni Kep Arizabalaga aliyepangua penalty mbili akitokea benchi.

4 – Ni idadi ya makombe ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya ambayo Lionel Messi ameshinda akiwa na klabu ya Barcelona huku kombe lake la mwisho kulitwaa la michuano hiyo lilikuwa lile walilomfunga Kibibi kizee cha Turin, Klabu ya Juventus mwaka 2015 mabao 3-1.

Licha ya kuwa miongoni mwa wachezaji waliowahi kutwaa kombe hilo mara nyingi lakini, Messi amesema ndoto yake kubwa kwasasa ni kutaka kushunda mataji mengine likiwemo la michuano hiyo amabyo ni mikubwa na yenye msisiimko mkubwa kwa ngazi za vilabu. Messi ameyasema hayo wakati alipokuwa anatambulishwa rasmi kwenye klabu yake ya sasa ya PSG.

3 – Ni idadi ya michezo aliyotoka sare bondia Manny Pacquiao raia wafilipino mwenye umri wa miaka 42 kwenye michezo yake 71 aliyocheza tokea miaka ya 90 na sasa kumfanya ashikilie nafasi ya nane kwa mabondia wenye ubingwa wa dunia.

Mkongwe huyo amekubali kuzichapa na Yordenis Ugas raia wa Cuba mwenye miaka 35 mape,a mwezi ujao baada ya kuzichapa na Errorl Spencer Jr kkwenye pambano lao lililopangwa kufanyika Agosti 21 mwaka huu kufuatia Spence JR kulazimika kufanyika upasuaji mdogo wa jino lake ambalo lilianza kumsumbua.

Pacquiao alipigana mara ya mwisho mwezi Julai 2019 alipompiga Keith Thurmanna kushinda ubingwa wa WBA welterweight ilhali Ugas mara ya mwisho alipigana mwezi Septemba mwaka jana na kumpiga Abel Ramos na kushinda ubingwa wa WBA Super champion.

2 – Ni idadi ya fainali ambazo klabu ya Azam imezicheza na kufanikiwa kuwa mabingwa wa mashindano ya CECAFA KAGAME CUP ilipo fanyika kwenye ardhi ya Tanzania huku mwaka 2012 ikiishia kutinga fainali pekee bila kuwa mabindwa.

Azam FC wameshindwa kuendeleza rekodi yao hiyo ya kibabe mara baada ya usiku wa jana kufungwa kwa penalty 4-2 na timu ya Nyassa Big bullets ya Malaw kufuatia sare ya 2-2 dakika 30 za niongeza. 

Baada ya matokeo hayo, Express itakipiga dhidi ya Nyassa Big Bullets tarehe 14 Agosti 2021kwenye fainali ilhali Azam watacheza na KMKM kuwania mshindi watatu.

1 – Ni nafasi anayoshikilia mwanamama Johanna Konta kwenye viwango vya ubora wa wachezaji tennis Duniani ambaye usiku wa kuamkia leo amefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Canadian Open baada ya kumfunga Elina Svitolina anayeshika nafasi ya tano kwa ubora kwa seti 3-6, 3-6 na 6-2.

Kwa matokeo hayo, sasa Konta atakutana na mrusi Anastazia Potapova au Mmarekani Coco Gaulf kwenye hatua hiyo ya mtoano inayofuata ya 16 bora. Michuano hiyo inataraji kurudisha utimamu na kiwango cha Konta kwasababu mkali huyo wa tennis alishindwa kushiriki michuano ya Wimbledon kutokana na kupata maambukizi ya Covid-19.

Chanzo: eatv.tv