Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Sports Countdown' leo, Yanga kuwakosa watatu

Djuma Pic Data Wachezaji wa Yanga watakaoikosa mechi ya hatua ya kwanza dhidi ya Rivers

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: eatv.tv

Sports Countdown' ya EA Radio leo Septemba 9, 2021, Yanga kuwakosa nyota wake watatu kisa kukosa vibali vya kimataifa vya kufanyia kazi nchini Tanzania 'ITC' wakati ambao Emma Raducanu avuna dola za kimarekani 675,000 sawa na Bilioni moja na zaidi ya milioni 500 za Kitanzania.

6 - Ni idadi ya mabao ya jumla ambayo klabu ya Yanga iliifunga timu ya Ngaya FC ya Visiwa vya Comoro mabo 6-2 mwaka 2017 kwenye hatua ya awali ya mtoano michuano ya klabu bingwa Afrika na kutolewa na Zanaco FC ya Zambia kwa sare ya 1-1 kwenye hatua ya mzunguko wa kwanza ya mtoano wa michuano hiyo ambapo ilipita miaka 4 bila Yanga kucheza michezo ya michuano hiyo.

Zikiwa zimesalia siku 3 kuelekea kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya Rivers United ya Nigeria wa hatua ya awali ya mtoano michuano ya klabu bingwa Afrika mchezo utakaochezwa Jumapili ya Septemba 12, 2021 kwenye dimba la Mkapa jijini Dsm, Msemaji wa Yanga Haji Manara amethibitisha baadhi ya nyota watatu wapo hatiani kuukosa mchezo huo.

Wachezaji hao ni Mlinzi wa kulia, Djumaa Shabani, Kiungo Khalid Aucho na Mshambuliaji Fiston Mayele ambao mpaka sasa hawajapata vibali vyao vya kimataifa kutoka shirikisho la soka barani Afrika CAF ili waruhusiwe kucheza michuano hiyo huku wakiwa na subra huenda vibali vikapatikana kabla ya mchezo huo.

5 - Ni idadi ya makundi yaliyochezwa usiku wa kuamkia leo katika michezo 13 ya kuwania kufuzu kombe la dunia kwa upande wa bara la ulaya ambapo vigogo wengi wamefanikiwa kuibuka na matokeo mazuri.

Bingwa wa UEFA EUROS timu ya Italy imeifunga Lithuania 5-0 Moise Keane akifunga 2 na kuifanya Italy kuzidi kutanua rekodi ya kuwa timu pekee kwa upande wa kimataifa kucheza michezo 37 mfululizo bila kufungwa. 

Kosovo 0-2 Hispania, Belarus 0-1 Ubelgiji, Iceland 0-4 Ujerumani, Timo Werner akifunga michezo 3 mfululizo ilhali England 1-1 Poland.

4 - Ni idadi ya vigogo ambao huenda wakawakosa wachezaji wake nyota kwenye michezo ya ligi kuu England itakayochezwa wikiendi hii kutokana na shirikisho la soka nchini Brazil kupeleka malalamiko FIFA kutaka iviadhibu vilabu vya Liverpool, Chelsea, Manchester United na Manchester City kwa kugomea kuwaruhusu wachezaji wake kujiunfa na timu yao ya Taifa ya Brazil.

Wachezaji hao ni Alisson Becker, Roberto Firmino, Fabinho wa Liverpool, Fred wa Manchester United, Thiago Silva wa Chelsea, Ederson, Gabriel Jesus & Zack Steffen wa Macnhester City.

Shirikisho la soka Brazil, Limezingatia kifungu cha 22 cha sheria za nidhamu za FIFA ambazo zimezuia vilabu kutowaruhusu wachezaji wake kucheza timu ya taifa na kufanya hivyo adhabu zake huwa ni wachezaji hao kufungiwa siku 5 kucheza mchezo wowote, timu kulimwa faini au klabu itakayowachezesha wachezaji hao basi watapokwa alama 3 wakipata ushindi na wapinzani wake watapewa alama 3 na mabao 3 kwa kosa la kuchezesha wachezaji waliofungiwa kwa muda huo.

3 - Ni idadi ya miaka iliyopita tokea klabu ya Mtibwa Sukari iwe bingwa wa kombe la Shirikisho nchini kwa kuifunga Singida United mabao 3-2.

Wakata miwa hao wa Manungu Turiani, mkoani Morogoro wamezidi kujiimarisha kuelekea msimu ujao wa Ligi kuu bara kwa kufanya usajili wa mlinzi wa kati wa Zamani wa Simba na Taifa Stars, Abdi Banda kwa mkataba ambao haukuwekwa wazi akitokea klabu ya TX Galaxy ya Afrika kusini.

Usajili wa Banda, ni usajili wa nne wa Mtibwa Sukari kwenye dirisha kubwa la usajili lililofungwa siku 9 zilizopita baada ya kumsajili kiungo Hamis Ndelwa kwa mkopo wa mwaka 1 akitokea Simba, Kiungo George Chota wa Mbeya City na winga wa kushoto Isaac Kachwele kutoka Cambiasso Sports Academy.

2 - Ni awamu anayoshiriki mwanadada Emma Raducanu kwenye michuano ya Tennis ya Grand Slam na tayari binti huyo mwenye miaka 18 ameweka rekodi za kibabe baada ya kumfunga Belinda Bencic wa Uswizi anayeshikilia nafasi ya 11 kwa ubora duniani kwa wanawake kwenye tennis seti 6-3 & 6-4 na kutinga nusu fainali ya US Open usiku wa kuamkia leo ilhali Emma alikuwa ni wa 150 na baada ya ushindi huo atasogea hadi nafasi ya 50 na 1 kwa wanawake England kwa sasa.

Rekodi za kibabe alizoziweka Binti Emma ni, mwanamke wa kwanza kwenye tennis kucheza michezo ya kuwania kufuzu US Open na kufanikiwa kufika nusu fainali, ni mwanamke wa kwanza Muingereza kufika nusu fainali ya US Open kwa mara ya kwanza tokea Jo Durie afanye hvyo mwaka 1983 na mwanamke wa kwanza kutoka England kufika nusu fainali ya US Open baada ya miaka 43 kupita.

Emma Raducanu amejizolea dola za kimarekani 675,000 sawa na Bilioni 1 na zaidi ya milioni 500 za Kitanzania kwa kufika hatua hiyo.

Sasa Emma Raducanu atacheza na Maria Sakkari jioni ya leo baada ya Maria kumtoa Karolina Pliskova.

Kwa upande wa wanaumez bingwa wa Tennis wa Olympic, Alexander Zverev atacheza na Novak Djokovic kwenye nusu fainali ya michuano hiyo endapo Djokovic atamtoa Matteo Berettini wa Italy.

1 - Ni namba ya jezi anayovaa mlinzi nyota wa timu ya taifa ya Canada ya mpira wa kikapu, Kevin Pangos ambaye muda mchache uliopita amesaini kandarasi ya miaka miwili kuichezea Cleveland Cavaliers mabingwa wa msimu juzi wa NBA baada ya kucheza kwa miaka 6 barani Ulaya kwenye timu ya Zenit St. Petersburg ya mpira wa kikapu.

Pangos mwenye miaka 28 alikiwasha huko Zenit akiwa na wastani wa kupata alama 14 na Assisti 7 hvyo kutegemewa sana kuongeza nguvu pamoja na Ricky Rubio ambaye amejiunga na Cavaliers akitokea Minnesota Timberwolves.

Chanzo: eatv.tv