Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sports Countdown, bilion 311 kumnunua Lukaku

Skysports Romelu Lukaku Inter Milan 5470869 Sports Countdown, bilion 311 kumnunua Lukaku

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Stori kali 6 za michezo kwenye Supa Breakfast ya East afrika radio leo Agosti 9, 2021. kila namba inahusiana na stori, na moja ya stori kubwa leo ni Chelsea ipo tayari kutoa zaidi ya bilioni 311 kwa Lukaku lakini pia hatma ya Simba day bado haijajulikana.

6. Ni idadi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu ya Yanga mpaka sasa katika kipindi hiki cha usajili, na idadi hiyo imefikia baada ya hapo jana timu hiyo ya wananchi kutoka mitaa ya twiga na Jangwani kutangaza kuwa imekamilisha usajili wa golikipa Diarra Djigui raia wa Mali kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na klabu ya Stade Malien ya Bamako Mali.

Mlinda mlango huyo anafanya idadi ya wachezaji walitambulishwa na kutajwa rasmi kuwa usajili wao umekamilika kufikia 6 akiunga na wachezaji wengine ambao ni Djuma Shaaban, Heritier Makambo, Fiston Mayele, David Bryson, na Yusuph Athuman.

Diarra Djigui pia anakuwa mchezaji wa 4 wa kigeni anajiunga na mabingwa hawa wakihistoria wa Tanzania sambamba na wakongo Djuma Shaaban, Fiston Mayele na HeritierMakambo.

 

5. Ni mataji ya EPL iliyotwaa klabu ya Chelsea chini ya mmiliki Bilionea Roman Abramovich na katika harakati za kuhakikisha wanatwaa tena taji hilo chini ya mmiliki huyo, klabu hiyo kutoka jiji la London inaripotiwa ipo tayari kutoa Pauni milioni 97 ambayo ni zaidi bilioni 311 kwa pesa za Tanzania kama ada ya uhamisho ya mshambuliaji Romelu Lukaku wa Inter Milan ya Italia.

Awali Chelsea ilikuwa ikimuwania mshambuliaji wa Dortmund Erling Braut Håland lakini klabu hiyo imeonesha nia yakutomuuza mshambuliaji huyo kinda ambaye ameshaifungia Dortmund mabao 60 kwenye michezo 60. Kwa mujibu wa Gazzetta Dello Sport limeripoti kuwa Lukaku yupo tayari kujiunga na Chelsea licha ya hapo awali kusisitiza kuwa anataka kubaki Inter na kushinda mataji zaidi.

Lukaku mwenye umri wa miaka 28 msimu uliopita alifunga jumla ya mabao 30 kwenye michezo 44 kwenye mashindano yote na kuisaidia Inter kutwaa ubingwa wa Ligi kuu Italia Serie A’ kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010. Na uvumi wa kuondoka Inter umezidi kuwa mkubwa baada ya kukosekana kwenye mchezo wa kirafiki hapa jana kati ya Inter Milan dhidi ya Parma mchezo ambao Inter ilishinda kwa mabao 2-0.

 

4. Ni mataji ya Ligi ya mabingwa barani ulaya aliyoshinda Lionel Messi akiwa na kikosi cha FC Barcelona na Mchezaji huyo bora wa Dunia mara 6 amesema anaamini walikuwa na nafasi ya kushinda taji hilo mara nyingi zaidi lakini bado anamatamanio yakutaka kushinda taji hilo kwa mara nyingine. Messi ametoa kauli hiyo alipokuwa akiongea na wanahabari juu ya kuondoka kwake katika klabu ya Barcelona baada ya miaka 21.

Kwenye sehemu ya hotuba yake La Purga amesema anaamini kwa kizazi ambacho kiliunda kikosi cha Barcelona ambacho alikuwa sehemu ya kizazi hicho kwa miaka kadhaa anaamini walikuwa na nafasi ya kushinda mataji mengi zaidi ya Ulaya kuliko manne waliyoshinda. Messi ameshinda jumla ya mataji 34 akiwa na Barcelona manne yakiwa ni ya klabu bingwa.

Kwenye mkutano huo aliweka wazi kuwa amepigiwa simu na timu nyingi ambazo zimeonyesha nia yakutaka kumsajili lakini kwa sasa anafanya mazungumzo na Klabu ya PSG ya Ufaransa. Na ripoti zinadai kuwa PSG itamtambulisha Messi ndani ya wiki hii.

 

3. Ni idadi ya mabao iliyofunga FC Barcelona kwenye mchezo wa Gamper trophy ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Juventus ya Italia. Mabao ya Barcelona yamefungwa na Memphis Depay, Martin Braithwaite na Riqui Puig. No Messi no Problem.

Mchezo huu ulikuwa wa mwisho kwa Barcelona kwenye michezo ya kirafiki ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi, na kocha Ronald Koeman alikuwa na kikosi cha wachezaji 21 kwenye mchezo huu huku wachezaji Clément Lenglet na Sergio Agüero hawakuwa sehemu ya mchezo kutokana na Majeruhi.

Ligi kuu nchini Hispania msimu wa 2021-22 utaanza kutimua Vumbi Agosti 13 na mchezo wa ufunguzi ni Valencia dhidi ya Getafe wakati Barcelona watatupa karata yao ya kwanza Agosti 15 dhidi ya Real Sociedad.

 

2. Ni tofauti ya dakika kati ya Eliud Kipchoge mshindi wa medali ya dhahabu kwenye Olimpiki kwenye mchezo wa riadha wa mbio ndefu za kilomita 42 yani Full marathon dhidi ya mtanzania Alphonse Simba aliyemaliza nafasi ya 7 kwenye mbio hizo zilizofanyika usiku wa kuamkia Jumapili huko Tokyo Japan. Kipchoge raia wa Kenya alitumia muda wa Masaa 2:8:38 wakati Simbu alitumia masaa 2:11:35 na kufanya tofauti ya dakika 2 na sekunde 57 kati ya Simbu na Kipchoge.

Simbu ameporomoka kwa nafasi 2 kutoka kwenye michezo ya Olympic iliyopita ya mwaka 2016 ambayo ilifanyika Rio de Jineiro Brazil ambapo alimaliza nafasi ya 5 na alitumia Masaa 2:11:15. Mtanzania mwingine aliyewakilisha upande wa wanaume Gabriel Geay alishindwa kumaliza aliishia kilomita 15 lakini Failuna Abdi Matanga kwa upande wa wanawake alimaliza nafasi ya 24 upande wa wanawake alitumia masaa 2:33:58.

 

1. Ni sawa na mwaka umepita tangu klabu ya Simba ilipofanya sherehe zake za Simba day, ambazo hufanyika Agosti 8 kila mwaka na Sherehe hizo zilipaswa kufanyika hapo jana lakini hazikufanyika ikiwa ni kwa mara ya kwanza sherehe hizo hazijafanyika tangu mwaka 2009 ambao siku hiyo ilianzishwa.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote kwa nini sherehe hizo hazijafanyika hapo jana na haijulikani kama mwaka huu shughuli hiyo itafanyika.

Simba day ilianzishwa miaka 12 iliyopita na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo kipindi hicho Hassan Dalali na katibu wake Mwina Kaduguda. Mahudhui ya siku hii ni kuwakutanisha wanasimba wote mashabiki, wanachama, viongozi na wachezaji ambapo kwenye siku hii hutambulisha wachezaji watakao iwakilisha Simba kwenye mashindano mbali mbali, Lakini pia hutambulisha jezi na namba ya kila mchezaji kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Chanzo: eatv.tv