Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sports Countdown, Taifa stars yapewa milion 10

241392342 1250153135437665 3897491182266138095 N Sports Countdown, Taifa stars yapewa milion 10

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: eatv.tv

Sports Countdown ya Eastafrica Radio, kwenye Supa Breakfast kuanzia Saa 1:15 Asubuhi yenye stori sita ambapo kila stori inatokana na tarakimu 6, kuanzia 1 mpaka 6. Na stori kubwa leo Taifa stars yapewa milioni 10 na Serikali.

6. Ni idadi ya roundi ambazo Bondia Tayson Fury amejinasibu atamchapa na kumaliza pambano ndani ya raundi hizo 6 kwenye pambano lake dhidi ya Anthony Joshua litakalo fanyika siku za mbeleni. Mabondia hawa wamekuwa wakitupiana maneno huku kila mmoja akijitapa kuwa ataibuka na ushindi pindi wawili hao watakapo panga uringo kuzichapa. Awali iliripotiwa kuwa mabondia hao walifikia makubaliano na pambano lao lilipaswa kufanyika mwezi Agosti 2021.

Mipango ya Pambano hilo iliharibika mara baada ya Bondia Deontay Wilder kutaka pambano lake la tatu dhidi ya Tayson Fury lifanyika ambalo lilikuwa kwenye mkataba wa mabondia hawa, na pambano lao litafanyika Oktoba 9 katika Dimba la T.Mobile Arena Nevada Marekani, wakati Joshua nae atapigana na Oleksandr Usyk Septemba 25 2021. Na mara baada ya mabondia hawa kupigana mapamano haya ndipo itakapo tangazwa pambano lao litafanyika lini lakini kwa asilimia kubwa litafanyika mwaka 2022.

 

5. Ni idadi ya mataji ya klabu Bingwa bara Afrika ambayo klabu ya ya TP Mazembe ya nchini Kongo imeshinda, na mabingwa hawa mara 5 wa Afrika ndio klabu itakayocheza na machampion wa Tanzania Simba SC kwenye tamasha la timu hiyo Simba Day litakalofanyika Septemba 19 mwaka huu katika Dimba la Benjamin mkapa.

Taarifa hii ilitangazwa rasmi hapo jana na klabu ya Simba, na mara ya mwisho timu hizi kukutana katika mchezo wa kimashindano ilikuwa msimu wa 2018-19 katika hatua ya robo fainali klabu bingwa Afrika na TP Mazembe ilifanikiwa kuiondoa Simba kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 kwenye michezo ya mikondo miwili.

 

4. Ni nafasi ambayo timu ya Biashara United Mara ilimaliza msimu uliopita kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara, na kuifanya timu hiyo kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika, na itakuwa ni kwa mara ya kwanza timu hiyo inashiriki katika michuano hii, na kikosi hicho kimeondoka nchini leo Alfajiri kuelekea nchini Djibouti ambako kitacheza mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali dhidi ya Dikhil.

Mchezo huu utacheza siku ya ijumaa September 10, majira ya Saa 10:00 Jioni kwa saa za hapa nyumbani, kikosi cha Biashara kimeondoka na wachezaji 20 na viongozi takribani 10.

 

3. Ni sawa na miaka mfululizo mcheza tennis namba 2 Duniani mrusi Daniel Medvedev anafuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Marekani US Open. Medvedev amefanikiwa kufanya hivyo baada ya kumnyuka Mholanzi Botic van de Zandschulp kwa seti 3-1, 6-3, 6-0, 4-6, 7-5. na katika hatua ya Nusu fainali atacheza na Felix Auger-Aliassime.

Na anatazamwa kama mpinzani wa karibu wa Djokovic kwenye michuano hii kwenye mbio za kuchukua ubingwa msimu huu ingawa mapema mwaka huu alifungwa na Novak katika mchezo wa fainali ya michuanp ya wazi ya Australia lakini pia miaka miwili iliyopita alifungwa kwenye fainali ya US Open na Rafael Nadal, kwa upande wa Novak atacheza mcheza wake wa robo fainali leo Saa 1:00 usiku dhidi ya Matteo Berretini.

 

2. Ni magoli aliyofunga mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann hapa jana na mabao hayo yalitosha kuipa Ufaransa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Finland kwenye mchezo wa kundi D wa kuwania kufuzu kombe la Dunia barani ulaya.

Mabao ya Griezmann ya dakika ya 25 na 53 yalimfanya kufikisha idadi ya mabao 41 na kuingia kwenye orodha ya wafungaji bora wa tutu wa Juu wa muda wote wa timu ya taifa hilo na idadi hiyo ya mabao inamfanya alingane na gwiji Michel Platini ambaye pia ana mabao 41, huku Kinara wa ufungaji akiwa Thierry Henry na mabao 51, Oliver Giroud nafasi ya pili mabao 46. Na Ushindi huo wa ufaransa pia ulikuwa wa kwanza baada ya kucheza michezo 5 pasipo kupata ushindi.

 

1. Ni nafasi inayomiliki timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars kwenye msimamo wa Kundi J ikiwa na alama 4 katika michezo ya kuwania kufuzu kombe la Dunia mwakani. Tanzania imekwea kileleni mwa msimamo wa kundi hilo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya timu ya taifa ya Madagascar na kuondoka na alama zote 3 katika mchezo uliochezwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Alama hizo 3 zimeifanya Tanzania kufikisha alama 4 sawa na Benini ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo, wafungaji wa mabao ya mchezo huo kwa taifa stars yamefungwa na Erasto Nyoni, Novatus Dismas,na Fei Toto, na yale ya Madagascar yalifungwa na Thomas Fontaine na Njiva Rokotohorimalala. Mara baada ya ushindi huo Waziri wa Habari sanaa utamaduni na Michezo mh innocent Bashungwa ameahidi kutoa sh Milioni 10 kama motisha baada ya ushindi huo.

Chanzo: eatv.tv