Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sports Countdown, Stars ni kibonde wa Madagascar

E9o AO3XMAEXc P Sports Countdown, Stars ni kibonde wa Madagascar

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: eatv.tv

Sports Countdown ya Eastafrica Radio, kwenye Supa Breakfast kuanzia Saa 1 :15 Asubuhi yenye stori sita ambapo kila stori inatokana na tarakimu 6, kuanzia 1 mpaka 6. Na moja ya stori kubwa leo ni Tanzania kuminyana na Magascar.

6. Ni idadi ya michezo ambayo timu ya taifa ya Madagascar imecheza pasipo kupata ushindi kwenye mchezo hata mmoja kwenye michezo yao sita (6) ya mwisho, wametoka sare michezo 2 na wamefungwa michezo 4. Na timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars ni wenyeji wa taifa hilo leo katika mchezo wa kundi J wa kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia zitakazo fanyika nchini Qatar mwakani 2022. Mchezo huu utachezwa katika Dimba la Benjamin Mkapa kuanzia majira ya Saa 10 jioni na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho la Soka nchini TFF mashabiki hawataruhusiwa katika mchezo huu ikiwa ni maelekezo ya shirikisho la soka ulimwengu FIFA katika harakati za kujikinga na Uviko 19.

Licha ya rekodi hiyo mbaya ya Madagascar katika michezo yao 6 ya mwisho, lakini pia Tanzania haijaifunga Madagascar katika michezo 6 ya mwisho waliokutana Stars imefungwa mara 3 na sare 3. Mchezo mwingine wa Kundi hili ulichezwa jana kati ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Benini na mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, hii ni michezo ya roundi ya pili ya Kundi J mchezo wa kwanza Tanzania ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi you Kongo wakati Madagascar ilifungwa na Benini 1-0.

5. Ni idadi ya wachezaji wapya ambao klabu ya KMC imewatambulisha mpaka sasa kuwa imewasajili kuelekea msimu mpya wa mashindano wa 2021-22, wachezaji waliotambulishwa na timu hiyo kutoka Kinondoni Dar es salaam ni Miraji Athumani kutoka Simba ambaye kajiunga kwa mkataba wa Mwaka 1, Hassan Kessy nae kasaini mwaka 1 akitokea Mtibwa Sugar, Golikipa Farouk Shikalo raia wa Kenya nae kajiunga kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga, na wachezaji Awesu Awesu na Iddi Kipagwile wamejiunga kwa mkopo wa msimu mmoja wote wakitokea Azam FC.

Kwa mujibu wa kocha msaidizi wa kikosi hicho cha Kino boys Habibu Kondo amesema baada ya kushindwa kufikia malengo yao ya kumaliza katika nafasi 4 za juu kwenye msimamo msimu uliopita, malengo ya msimu huu ni kutwaa ubingwa ligi kuu soka Tanzania bara.

4. Ni sawa na masaa ambayo yalitosha kuifanya Jezi namba 7 ya Manchester United itakayovaliwa na Cristiano Ronaldo kuweka rekodi ya mauzo kupitia mtandao kuwa ndio jezi iliyonunuliwa zaidi kwa siku moja, ukitoa bara la Amerika ya Kaskazini. Baada ya Jumatano iliyopita Manchester United kutangaza kuwa Ronaldo atavaa Jezi namba 7 uhitaji wa Jezi hiyo umekuwa mkubwa ambapo watu wamekuwa wakinunua kupitia mtandao yani (Online) lakini pia mashabiki wamekuwa wakifika katika maduka tofauti tofauti kununu jezi hiyo na ndani ya masaa 4 tu ikaweka rekodi yakuwa Jezi namba iliyonunuliwa zaidi ndani ya masaa 24..

Jezi ya Ronaldo imekuwa ndio jezi iliyonunuliwa sana ndani ya masaa 24 ikifuatiwa na ya Messi baada ya kukamilisha usajili wakujiunga na PSG na ile ya LeBron James baada ya kujiunga na LA Lakers.  

3. Ni idadi ya Set alizoshinda Novak Djokovic kwenye mchezo wa roundi ya nne na kumfanya kufuzu robo fainali ya michuano ya wazi ya tennis ya Marekani US Open, baada ya kumfunga kinda wa Marekani Jenson Brooksby mwenye umri wa miaka 20. Djokovic ambaye ndio mchezaji namba 1 kwenye viwango vya ubora kwa wanaume alipoteza seti ya kwanza kwa 6-1 kabla ya kushinda seti 3 mfululizo kwa 6 -3 6-2 6-2.

Na katika hatua ya robo fainali atacheza dhidi ya Matteo Berretini ambaye aliminyana nae kwenye mchezo wa fainali ya Wimbledon mwezi Mei mwaka huu, Berrettini ambaye alicheza nusu fainali ya michuano hii mwaka 2019 ametinga hatu hii baada ya kumfunga mjerumani Oscar Otte kwa set 3-1 kwa 6-4, 6-3 6-2 na Otte alishinda seti ya pili kwa 6-3.

2. Ni idadi ya watoto ambao staa wa Zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na Vilabu vya PSG, na Nice Jean-Pierre Adams alijaaliwa kuwapata na mkewake Bernadette watoto hao ni Laurent ambaye alizaliwa mwaka 1969 na Frédéric aliyezaliwa1976. Na hapo jana Beki huyu wa zamani wa kati raia wa Ufaransa mwenye asili ya Senegal alitangazwa kuwa amefariki Dunia akiwa na miaka 73 baada ya kuwa kwenye Coma kwa kipindi cha miaka 39 kutokana na mwili wake wote kupalalaizi mwaka 1982.

Jean-Pierre alikutwa na tatizo hilo baada ya madaktari kufanya makosa wakati wakimfanyia upasuaji wa pili kwenye goti lake ambapo walizidisha dawa ya ganzi ambayo ilisababisha madhara kwenye ubongo wake na kusababisha kupalalaizi mwili mzima hivyo kwa kipindi cha miaka 39 amekuwa kwenye chamba cha uangalizi Coma akiwa haongei wala kuona kwa kipindi chote hicho mpana umauti unamfika hapo jana. Kwa mujibu wa takwimu Jean-Pierre Adams alicheza zaidi ya michezo 285 na alifunga mabao zaidi ya 26. Hakika Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi Amini.

1. Ni bao pekee ambalo alifunga mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Willian katika michezo 37 akiwa na kikosi cha washika bunduki wa jiji la London klabu ya Arsenal msimu uliopita wa 2020-21, mchezaji huyo ameweka wazi kuwa hakuwa na furaha katika klabu hiyo na ndio sababu iliyomfanya avunje mkataba na klabu hiyo baada ya miezi 12 tu, licha yakuwa ilikuwa imesalia miaka miwili (2) kwenye mkataba wake. Willian mwenye umri wa miaka 33 amesema hawezi kuweka wazi ni vitu gani ambavyo vilimfanya akose furaha lakini aliishi nje ya matarajio yake.

Willian alijiunga na Arsenal akiwa mchezaji huru akitokea Chelsea katika dirisha la usajili la majira ya Joto msimu uliopita na alisaini mkataba wa miaka mitatu ambao ulikuwa unamlipa pauni laki mbili na elfu ishirini kwa wiki kama mshahara wake. Mara baada ya kuvunja mkataba na the Gunners Willian amejiunga na timu ya nyumbani kwao Brazil Corinthians ambayo ndio aliyoanza kuichezea akiwa mchezaji kinda, anarejea nchini Brazili baada ya miaka 8 ya kucheza soka nchini England.

Chanzo: eatv.tv