Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sports Countdown, Messi amesaini miaka miwili PSG

234628825 545763256742716 3962732985620760149 N Sports Countdown, Messi amesaini miaka miwili PSG

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

Stori kali 6 za michezo kwenye Supa Breakfast ya East afrika radio leo Agosti 11, 2021. kila namba inahusiana na stori, na moja ya stori kubwa leo ni Simba kuweka kambi ya maandalizi ya msimu nchini Morocco, Messi asaini miaka miwili PSG.

Submitted by George David on Jumatano , 11th Aug , 2021 Lionel Messi kushoto amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya PSG.

6. Ni nafasi ambayo alishika mshambuliaji wa Mancheater United Marcus Rashford kwenye orodha ya wachezaji waliotoa pasi za magoli (Assist) kwenye Ligi Kuu England EPL msimu uliopita, ambapo alipiga pasi hizo 9.

Na hapo jana mchezaji huyo alithibitisha kuwa upasuaji wake wa bega aliofanyiwa siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita ulifanyika salama, Rashford alikuwa akisumbuliwa na bega hilo Tangu mwezi Novemba mwaka jana na ililazimisha mchezaji huyo kuchoma sindano za kupunguza maumivu kabla ya mwezi uliopita kufikia uamuzi wa kufanya upasuaji baada ya makubaliano na Kocha Ole Gunnar Solskajer na jpo la Madaktari.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili akitibu bega hilo na anatarajiwa kurejea uwanjani mwezi Oktoba na atakosa michezo taklibani saba ya mwanzoni mwa msimu, na Ligi Kuu England EPL inaanza wiki hii na Manchester United mchezo wake wa kwanza itacheza Jumamosi dhidi ya Leeds United.

5. Ni muda unaotarajiwa klabu ya PSG ya Ufaransa itamtambulisha mchezaji bora wa Dunia mara 6 Lionel Messi mbele ya wanahabari leo asubuhi, hii ni mara baada ya usiku wa jana timu hiyo kutoka jiji la Paris kutangaza kuwa Messi amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili (2), huku ikiripotiwa kuwa mkataba huo una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja na matajiri hao wa jiji la Paris watamlipa La Purga mshahara wa Euro milioni 35 kwa mwaka ambayo ni zaidi ya bilioni 95 kwa pesa za kitanzania.

Messi aliwasili katika jiji la Paris Ufaransa hapo jana akiwa na familia yake mkewake na watoto zake watatu. Usajili wa Messi katika klabu ya PSG utakuwa ni usajili mwingine mkubwa kufanywa na klabu hiyo baada ya kukamilisha usajili wa Gianluigi Donnarumma, Sergio Ramos, Achraf Hakimi na Georginio Wijnaldum, maboresha haya ya PSG chini ya kocha Mauricio Pochetino yanazidi kuipa kipaumbele timu hiyo kuwa kwenye nafasi ya kutwa taji la klabu bingwa ulaya (UEFA champions league ) msimu ujao kombe ambalo timu hiyo haijawahi kushinda na inatajwa kuwa ubingwa wa michuano hiyo ndio kipaumbele cha wamiliki wa timu hiyo.

4. Ni idadi ya mataji ya Ligi kuu Tanzania bara mfululizo iliyotwaa klabu ya Simba na katika jitihada za kuhakikisha wanazidi kujiimarisha kutetea ubingwa kwa mara ya 5 klabu hiyo kutoka mitaa ya Msimbazi Kariakoo imeondoka nchini jana kuelekea mchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao yani pre season.

Kwa mujibu wa taarifa mabingwa hao watanzania wataweka kambi ya wiki mbili na watacheza michezo kadhaa ikiwa ni nafasi yakujiweka sawa kueleka msimu wa mashindano ambapo watashiriki kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika watakuwa na kibarua cha kutetea ubingwa wa Tanzania bara na kutetea ubingwa wa kombe la Azam Sports Federation Cup.

3. Ni idadi ya wachezaji waliosajiliwa na klabu ya Biashara mara United ya mkoani Mara katika dirisha hili la usajili, wachezaji hao ni Atupele Green aliyejiunga na timu hiyo akitokea Geita Gold na amesaini mkataba wa mwaka mmoja (1), mchezaji mwingine ni Tayo Odongo Matthew amejiunga kwa mkataba wa miaka miwili (2) kutoka timu ya Zoo football ya Kenya na mchezaji wa tatu ni Aniset Revorcutous Kezilahabi kwa mkataba wa miaka miwili (2) akitokea Mwadui FC.

Biashara Unite itaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika na itakuwa kwa mara ya kwanza timu hii inashiriki mashindano hayo na walikata tiketi hii baada ya kumaliza nafasi ya nne msimu uliopita.

2. Ni idadi ya wanamichezo watakao iwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu Paralympic itakayofanyika Tokyo Japan kuanzia Agosti 24 mwaka huu mpaka Septemba 5. Na wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michezo hiyo ni Sauda Njopeka na Igginas Mteve na wataondoka nchini siku ya Ijumaa Agosti 13 kuelekea Japani.

Katibu mkuu wa kamati ya michuano ya Paralympic Tanzania Ramadhani Namkoveka amesema kuwa katika michuano hiyo mikubwa dunia Tanzania tutashiriki kwenye mchezo wa wakurusha Tufe na kisahani na wanaamini wawakilish hao ambao wanakwenda kuiwakilisha nchin watarudi na medali.

1. Ni kombe pekee la michuano ya Uefa Super Cup iliyoshinda klabu ya Chelsea na matajiri hao kutoka jiji la Londo watakuwa wakiwania kushinda taji hilo kwa mara ya pili ambapo leo usiku majira ya Saa 22:00 usiku wataminyana na Villarreal ya Hispania kwenye mchezo huo wa Uefa Super Cup.

Mchezo huu unazikutanisha timu mbili ambazo ni mabaingwa wa michuano ya vilabu barani ulay klabu bingwa (ulaya Uefa champion league) ambao ni Chelsea na walitwaa ubingwa kwa kuinyuka Manchester City kwenye mchezo wa fainali kwa bao 1-0 na wapinzani wao ni Villarreal ambao ni mabingwa wa Uefa Europe League ambao walitwa ubingwa kwa kuifunga Manchester United kwa mikwaju ya penati.

Hii inakuwa ni mara ya tano kwa Chelsea kucheza kwenye mcgezo wa Uefa Super Cup mara nne (4) zilizopita wameshinda mara 1 ilikuwa dhidi ya Real Madrid mwaka 1998 kwa bao 1-0 na wamepoteza michezo mingine mitatu, wakati kwa Villarreal ni mara ya kwanza kucheza mchezo wa UEFA Super Cup.

Chanzo: eatv.tv