Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sports Count down ya EA Radio Agosti 6

Lionel Messi Sports Count down ya EA Radio Agosti 6

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: eatv.tv

'Sports Countdown' ya EA radio ya leo Agosti 6, 2021 kuhesabu zile stori sita kali za kimichezo ndani na nje ya nchi. Kubwa zaidi ni mshambuliaji Lionel Messi kushindwa kusajiliwa Barcelona na wawili hao kuachana rasmi na Messi kuwa mchezaji huru PSG na Manchester City wakihusishwa.

6 - Ni idadi ya tuzo za mwanasoka bora wa dunia 'Ballon D'or' alizoshinda Mshambuliaji hatari, Lionel Messi na kumfanya kuwa mchezaji pekee aliyetwaa tuzo hizo mara nyingi zaidi kwenye historia ya tuzo hizo huku mpinzani wake Cristiano Ronaldo ikitwaa mara 5.

Taarifa ya kushtusha na yakusikitisha kwa mashabiki wa Barcelona zilithibitishwa na klabu ya FC Barcelona yenyewe usiku wa jana kwa kuweka wazi kuwa nyota huyo hatoichezea klabu hiyo tena baada ya klabu kuwa na ukata na kukutana na kuzuizi kutoka La Liga vinayodhibiti kima cha mishahara kwa wachezaji.

Messi anaondoka klabu hapo akiwa shujaa wa mfano kwani tokea acheze mchezo wake na timu ya wakubwa mwaka 2003 hadi 2021 amefanikiwa kucheza michezo 778, kufunga mabao 672 na ku-assist mabao 305 na kuwa mchezaji pekee aliyehusika kwenye bao mengi FC Barcelona, mabao 977 kwenye michezo 778 na kubeba mataji 35.

5 - Ni idadi ya michezo aliyocheza kiungo mchambuliaji wa timu ya taifa ya England, Jack Grealish kwenye michuano yw UEFA EUROS iliyomalizika mwezi uliopita na kutoa assist mbili na kuisaidia timu yake kutinga fainali na kupoteza mbele ya Italy kwa mikwaju ya penalti.

Nyota ya kiungo huyo mwenye uhodari wa kudemka na mpira imezidi kung'aa kwani usiku wa kuamkia leo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kusajiliwa kwenye historia ya EPL baada ya kusajiliwa na mabingwa watetezi wa ligi hiyo klabu ya Manchester City kwa ada ya rekodi paundi milioni 100 sawa na zaidi ya bilioni 320 za kitanzania na kusaini mkataba wa miaka 5 hadi 2026 akitokea klabu yake ya utotoni, Aston Villa aliyodumu nayo kwa zaidi ya miaka 16.

Ikumbukwe kuwa rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na kiungo Paul Pogba alivyosajiliwa kwa paundi mil 85 kutoka Juventus mwaka 2016.

4 - Ni idadi ya rebound alizopiga nyota wa timu ya taifa ya kikapu ya Marekani, Drummond Green kwenye mchezo wa nusu fainali ya Olympic ambao ulimalizika kwa USA kushinda kwa alama 97-78 dhidi ya Australia huku mchezo wa nusu fainali ya pili Ufaransa alimfunga Slovenia kwa alama 90-89.

Baada ya matokeo hayo, timu ya taifa ya USA ambao ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo kwa kushinda mara 15 katika mara 18 walizoshiriki, watakipiga dhidi ya Ufaransa kwenye fainali ya mchezo huo wa mpira wa kikapu kwa wanaume siku ya Agosti 7 mwaka huu saa 11:30 jioni ilhali Slovenia na Australia watacheza mchezo wa kuwania mshindi watatu siku hiyo hiyo saa 8:00 mchana.

3 - Ni idadi ya michezo waliyokutana timu ya taifa ya Mexico na Japan tokea mwaka 1986 ambapo Mexico wameibuka wababe mara mbili ilhali Japan walishinda mchezo mmoja huku mara ya mwisho kwa wawili hao kukutana ikiwa ni Julai 27 mwaka huu kwenye mchezo wa makundi wa michuano hii ya Olympic.

Wawili hao wanataraji kushuka tena dimbani Saa 6:00 mchana wa leo kwenye uwanja wa Saitama nchini Japan kukipiga kwenye mchezo wa soka kuwania nafasi ya mshindi watatu ambaye atapata medali ya shaba.

Brazil na Hispania wao watakipiga kesho Agosti 7, kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Olympic kwa upande wa soka kuwania medali ya Dhahabu.

2 - Ni idadi ya medali za dhahabu walizoshinda wana masumbwi kutoka nchini Cuba kati ya tatu walizokuwa wanashindania kwenye michuano hii ya Olympic inayoendelea nchini Japan na kuwaacha wenyeji wakiambulia medali moja ya dhahabu.

Cuba wamepata medali hiyo baada ya bondia wake, Arlen Lopez mwenye umri wa miaka 28 kumsukumia makonde na kumdunda bondia Mwingereza, Ben Whittaker mwenye umri wa miaka 25 na Lopez kushinda fainali hiyo ya uzito wa juu wa kilo 75-81 hapo jana.

Whittaker baada ya kudundwa aligoma kuvaa medali yake ya fedha kwa kuwa mshindi wa pili na kuiweka mfukoni huku akisema amefanya hvyo kwasababu kushinda medali hiyo haikuwa ndoto yake huku wengine wakikitafsiri kitendo hicho kama dharau.

1 - Ni idadi ya mchezaji anaye cheza kwenye nafasi ya ulinzi ambayo klabu ua Tottenham Hotspurs inaelezwa itamsajili na hii ni baada ya kumuweka Sokoni mlinzi wake Davinson Sanchez raia wa Colombia.

Spurs imethibitisha hilo licha ya kumsajili mlinzi mpya wa kati usiku wa kuamkia leo, Crisitiano Romero raia wa Argentina mwenye miaka 23 kwa kandarasi ya miaka 5 kwa ada ya uhamisho paundi milioni 47 za England sawa na zaidi ya bilioni 90 za kitanzania.

Cristian Romero anakuwa mchezaji wapili kusajiliwa kwa kiasi kikubwa kwenye historia ya klabu ya Spurs baada ya Tanguy Ndombele kusajiliwa kwa paundi milioni 54 za England sawa na zaidi ya bilioni 150 za Kitanzania mwezi Julai 2019 akitokea klabu ya Lyon ya Ufaransa.

Chanzo: eatv.tv