Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SportPesa wazindua kituo kikubwa cha huduma kwa wateja Tanzania (+Video)

Thu, 1 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Kampuni ya kubashiri michezo nchini Tanzania ya SportPesa leo Alhamisi Februari 01, 2018 imezindua kituo kikubwa zaidi cha Huduma kwa Wateja nchini Tanzania ili kutatua matatizo mbalimbali ya wateja wao.

Mkurugenzi wa  Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania, Ndg Tarimba Abbas.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam katika Ofisi za makao makuu ya Kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa Tanzania, Ndg Tarimba Abbas amesema mbali na kitengo hicho kusaidia wateja wao pia kimetoa ajira kwa Watanzania 84 huku akieleza kuwa kituo hicho ni kikubwa zaidi nchini kuliko vituo vyote vinavyotumiwa na makampuni mengine ya kubeti.

Kutokana na moja ya changamoto kubwa ambazo vijana wanapitia ni ajira, sisi kama SportPesa tumeajiri vijana wapatao 84 wakitanzania kwenye kitengo chetu cha Huduma kwa Wateja na vijana hawa wamefanyia mafunzo nchini Kenya na wamepata uzoefu wa kutosha,“amesema Tarimba.

Kwa wateja wa SportPesa au wale wanaotaka kujua zaidi huduma za kampuni hiyo unaweza kupiga simu hizi 0764 115588, 0692 115588 au 0685115588 na simu hizi zinapatikana masaa 24.



 

Chanzo: bongo5.com