Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SportPesa inavyojivunia kuleta maendeleo ya soka Tanzania

12854 Pic+spotpesa TanzaniaWeb

Mon, 20 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kampuni inayoongoza ya michezo ya kubahatisha nchini, SportPesa Tanzania inajivunia kuchangia maendeleo ya soka tangu ianze kufanya shughuli zake nchini.

SportPesa Tanzania ilianza kufanya biashara nchini Mei mwaka jana na mara moja ikasaini mkataba wa miaka mitano kila moja na wakongwe wa soka, Yanga na Simba.

Wakati Simba ikisaini mkataba wa miaka mitano wenye dhamani ya Sh 4.9 billioni, Yanga ilisaini mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Sh 5 billioni. Mikataba hiyo itamalizika msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wa mwaka 2021/22.

Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas alisema kuwa malengo ya kusaidia maendeleo ya soka na sekta nyingine yameanza kuleta mafanikio klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya miaka kadhaa huku Yanga ikifanikiwa kuingia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho.

Alisema kuwa makocha na wachezaji vijana kadhaa wamefaidika kupitia shughuli zao mbalimbali nchini ikiwa pamoja na mafunzo yaliyoendeshwa na gwiji wa klabu ya Everton, Leon Osman.

“Kuna maendeleo ya soka nchini tangu tuanze shughuli zetu na klabu zimefaidika na wachezaji wameona mwanga wa kazi yao, ninaamini maendeleo zaidi yatapatikana kwani tumejipanga kufanya hivyo ili kufikia malengo yetu,” anasema Tarimba.

ZIARA YA EVERTON TANZANIA

Tarimba anasema kuwa ili kuleta hamasa kwa wachezaji, viongozi na mashabiki, kampuni yao iliandaa ziara ya Everton ambayo iliundwa na wachezaji nyota wa mataifa mbalimbali ikiwa pamoja na Wayne Rooney ambaye alikuwa amejiunga na timu hiyo.

Mashabiki wa soka hawakuamini kama timu hiyo na mastaa hao watakuja kucheza na mshindi wa mashindano ya SportPesa Super Cup na timu ya Gor Mahia ya Kenya ilishinda na hatimaye kucheza na Everton Uwanja wa Taifa.

Mashabiki wa soka walipata hamasa kuiona timu hiyo ikicheza kwa mara ya kwanza nchini ikiwa na wachezaji nyota. Ziara hiyo imeleta mtazamo chanya kwa soka ya Tanzania kuwa inawezekana kucheza soka nje ya nchi kutokana na vipaji vya wachezaji.

“Ziara ya Everton imeleta faida nyingi, ikiwa pamoja na kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, kukuza utalii na pia kufanyia msukumo wa ukarabati Uwanja wa Taifa na kuwa wa kisasa duniani,” anasema Tarimba.

Anasema kuwa wachezaji wa Everton pia walishiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa pamoja na kutembelea hospitali ya Watoto ya Pugu, kuendesha mafunzi kwa klabu ya albino na mambo mengine.

TUZO

Mpaka sasa, kampuni yao imeshindanishwa katika tuzo mbalimbali ikiwa pamoja na tuzo ijulikanayo kwa jina la United Kingdom (UK) Business Football Awards na ile ya Best Brand Activation.

Kushindanishwa huko kumetokana na ushiriki wa kampuni hiyo kwa timu maarufu kama , Everton FC na ile ya Daraja la Kwanza (EFL Championships), Hull City Tigers.

Kampuni hiyo pia imeshindanishwa katika tuzo ijulikanayo kwa jina la Discovery Sport Industry Awards ambayo itafanyika leo (Agosti 17), kwenye ukumbi wa Sandton Convention Center, mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

SportPesa pia imeshindanishwa katika kipengele bora cha udhamini katika bara la Afrika (The Best African Sponsorship).

SHUGHULI ZA KIJAMII

Mbali ya kujihusisha masuala ya michezo, kampuni ya SportPesa pia imewekeza katika masuala ya afya kwa kujenga hospitali itakayotumiwa na madaktari wawili wa kitongoji cha Kizimkazi Mkunguni, Zanzibar.

Mradi huo tayari umemvutia Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan ambaye ameipongeza kampuni hiyo baada ya kutembelea mradi huo.

Chanzo: mwananchi.co.tz