Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sonso ashtukia jambo Yanga

68602 Pic+mtoni

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

ALLY Mtoni 'Sonso' aliyetua Yanga msimu huu akitokea Lipuli ameshtukia jambo katika kambi ya timu hiyo iliyopo Morogoro, akidai mpaka sasa hakuna nyota mwenye uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza na hivyo inamfanya ajifue zaidi ili kuridhisha makocha.

Akizungumza na MCL Digital, Sonso alisemani mapema sana kujiaminisha kuwa tayari amejitengenezea nafasi kikosini kwa kuweka wazi kuwa ushindani uliopo ni mgumu.

"Kuna wachezaji hadi sasa haijajulikana wanacheza nafasi gani huwezi kuamini ni mejifunza mengi nikiwa huku kwanmi tayari nimeshaona umuhimu wa kucheza nafasi nyingi uwanjani ili uweze kujihakikishia namba kwani hata ukishiundwa beki unaweza kucheza winga," alisema na kuongeza;

"Umakini ndio kitu kikubwa ambacho nakiamini na ndio siri ya mafanikio katika kazi yangu ya soka naamini kupitia hili naweza kupata mafanikio makubwa hasa katika klabu yangu hii kubwa ambayo natarajia kuichezea msimu mpya."

Sonso alisema kama Yanga itaendeleza ushindani uliopo kambini hadi katika ligi basi wanaweza kuwa na msimu mzuri na kuwa timu tishio msimu ujao huku akibainisha kuwa kila mchezazi yupo katika hari anapambana kuonyesha nini anacho kwa kocha ili aweze kumpa nafasi.

Chanzo: mwananchi.co.tz