Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Snoop Dogg kubeba Mwenge wa Olympic

Snoop Dogg Walkin 6253 Trials24 1200x675 Snoop Dogg kubeba Mwenge wa Olympic

Wed, 24 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa maarufu wa Marekani Snoop Dogg ataubeba Mwenge wa Olimpiki katika hatua za mwisho za safari ya mwenge huo kabla haujapelekwa kwenye kivutio maarufu cha Eiffel Tower kilichopo jijini Paris, Ufaransa.

Snoop ambaye jina lake halisi ni Calvin Broadus Jr, yuko jijini Paris kama mwandishi maalumu wa NBC ambalo ni mshirika wa Shirika la habari la Sky.

Kupitia mtandao wa X, Snoop (52) ameshea picha yake akiwa nje ya hoteli iliyoambatana na maneno ” Mko tayari? Paris 2024 Olympics...”.

Rapa huyo ataubeba mwenge huo kupitia kitongoji cha Saint-Denis ambapo kutafanyika tamasha ikiwa ni kituo cha mwisho kabla ya mwenge huo kuelekea Eiffel Tower.

Mwenge huo uliwashwa mwezi Aprili nchini Ugiriki, katika eneo ambalo ndipo ilipozaliwa michezo ya Olimpiki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live