Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Singida Utd yataka Ligi Kuu Bara ifutwe

18422 Pic+singida Singida Utd yataka Ligi Kuu Bara ifutwe

Mon, 11 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HUKU timu yake ikipewa nafasi kubwa ya kushuka daraja kutokana na kuburuza mkia kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Singida United, Ramadhan Nsanzurwimo, amesema kwa upande wake anaona ni bora ligi hiyo ifutwe msimu huu.

Singida United ipo mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 15 zilizotokana na mechi 29 ilizocheza hadi Ligi Kuu inasimama Machi 17, mwaka huu kutokana na mlipuko wa maambukizo ya virusi vya corona 9 (COVID-19).

Wiki iliyopita Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Almas Kasongo, alisema endapo serikali itatoa baraka za kuendelea kwa michezo nchini wanatarajia Ligi Kuu kurejea mapema Juni mwaka huu, jambo ambalo Nsanzurwimo hataki kuona likitokea.

Akizungumza na Nipashe jana, Nsanzurwimo alisema haoni sababu ya kurejesha kwa Ligi Kuu mapema kabla ya ugonjwa wa COVID-19 kumalizika hasa kutokana na mazingira ya mchezo huo ulivyo ambapo wachezaji hucheza na kufikia hatua ya kugusana na kutokuwapo kwa umbali unaotakiwa.

"Kwa upande wangu naona bora ligi ifutwe, hakuna bingwa wala kushuka daraja, mwakilishi wa kimataifa atachukuliwa yule bingwa wa Ligi Kuu na FA wa msimu uliopita," alisema kocha huyo.

Alisema endapo TPLB watashindwa kufuata, hivyo wasubiri janga hilo liishe na baadaye kupata muda wa makocha kuandaa timu zao ili kurejea uwanjani kumalizia msimu.

"Kama ligi itarudi muda huu, itawalazimu TFF na Bodi kutoa muda wa mwezi mmoja au miwili kwa ajili ya timu kufanya mazoezi, kwa sababu sasa hivi hatuelewi kama wachezaji wetu wanafanya mazoezi ipasavyo," alisema.

Nsanzurwimo alisema pia suala la kucheza mechi bila mashabiki ni adhabu kubwa kwa wachezaji pamoja na timu kutokana na asilimia kubwa ya klabu hutegemea mapato ya mlangoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live