Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simon Msuva hashikiki kwa mwendo huu Morocco

760 Wewew1 660x400 TZW

Fri, 29 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadid ya Morocco Simon Msuva anazidi kuchukua headlines kutokana na kasi na mchango wake anaozidi kuutoa katika club yake ya Difaa El Jadid.

Simon Msuva kwa mara ya pili anafanikiwa kuifungia timu yake goli muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu Morocco, Msuva leo ameipatia ushindi wa goli 1-0 timu yake ya Difaa El Jadid dakika ya 52 dhidi ya Hassania Agadir.

Kufunga kwa goli hilo kunamfanya Simon Msuva kusogea katika msimamo wa ufungaji bora kwani goli dhidi ya Agadir limemfanya kutimiza jumla ya magoli 5 na mtu anayeongoza ana magoli saba lakini huu ni mchezo wa pili kwa Msuva kufunga mfululizo.

#Tunamshukuru kwa kila jambo

Chanzo: millardayo.com