Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbu ashinda 21 km Rock City Marathon, Giniki aambulia nafasi ya tatu

Felix Simbu Simbu ashinda 21 km Rock City Marathon, Giniki aambulia nafasi ya tatu

Sun, 24 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MWANARIADHA wa Tanzania, Alphonce Simbu ameendeleza makali yake baada ya kuibuka mshindi wa kwanza mbio za Rock City zilizofanyika leo jijini Mwanza zikishirikisha wanariadha mbalimbali kutoka Tanzania, Kenya na Uganda.

Simbu ameshinda mbio za Kilometa 21 kwa wanaume  baada ya kutumia saa moja dakika sita na sekunde 19 na kujinyakulia Sh 2 milioni na medali ya Dhahabu, huku Mwanariadha wa Kenya Bernad Msau aliyetumia saa moja dakika Saba na sekunde sita akiibuka mshindi wa pili na kupata Sh 1.3 milioni na medali ya fedha.

Mtanzania mwingine Shingade Giniki aliibuka mshindi wa tatu baada ya kukimbia mbio hizo kwa saa moja dakika Saba na sekunde 35 na kujinyakulia Sh 700,000 na medali ya Shaba, huku Alexander Cheproton wa Kenya akiibuka wa nne kwa kutumia saa moja na dakika 12 akipata Sh 500,000.

Allan Kipruto wa Kenya alishinda nafasi ya tano akitumia saa moja dakika 12 na sekunde 14, Ludega Robert wa Uganda akishinda nafasi ya sita huku Watanzania waking'ara tena katika nafasi ya Saba hadi ya 10 n kujinyakulia Sh 100,000 kila mmoja na medali ya Shaba.

Kwa upande wa Wanawake Kilometa 21, Mkenya Isgan Cheluto aliibuka mbabe baada ya kutumia saa moja dakika 17 na sekunde 31, huku nafasi ya pili hadi ya 10 zikibebwa na Watanzania.

Neema Masuali alishika nafasi ya pili kwa kutumia saa moja dakika 23 na sekunde sita, Tunu Andrew akishika nafasi ya tatu akitumia saa moja dakika 25 na sekunde 17, Angel John nafasi ya nne (1:26:20) na Sarah Ramadhan nafasi ya tano akitumia saa moja dakika 29 na sekunde 21, ambapo washindi kuanzia nafasi ya tano hadi ya 10 walipata Sh 100,000 na medali ya Shaba kila mmoja.

Mmoja ya wadhamini wa mbio hizo, Emmanuel Mzava kutoka benki ya KCB amesema wametoa hamasa kwenye mashindnao hayo ili kutoa ajira, kutengeneza mahusiano, kukuza uchumi na biashara na kuimarisha afya, ambapo mbio hizo ni kivutio kwani kinakutanisha watu wengi ambapo washindi wote wataweza kutembelea kisiwa cha Saa Nane.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz