Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbu apongeza vipaji riadha wanawake

Alphonce Simbuuuuuuuuu.jpeg Simbu apongeza vipaji riadha wanawake

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha mwenye sifa ya kuipeperusha vema bendera ya Tanzania kimataifa, Alphonce Simbu, ameeleza kubaini vipaji vingi kupitia mashindano ya wanawake ya mchezo wa riadha (Ladies First), ambayo yamemalizika Dar es Salaam jana.

Akizungumza na gazeti hili jana jijini Dar es Salaam jana, Simbu alisema Tanzania ina wanariadha wengi chipukizi ila tatizo wanashindwa kutoka kutokana na kukosekana kwa wawezeshaji.

"Mashindano haya yanaushindani, kila mchezaji ameonyesha kipaji chake, ninaamini mashindano yajayo tutapata wanariadha ambao watashiriki mashindano mengine makubwa," alisema Simbu.

Aidha, alisema wanawake wakiwezeshwa wanaweza na kuwataka wazazi kuruhusu watoto wao wa kike wajitokeze kwenye michezo.

Mashindano hayo yalishirikisha mikoa 31 kutoka Tanzania Bara na Visiwani ambapo wanariadha 186 walishiriki kwenye mbio kuanzia mita 100 hadi10,000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live