Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbu apigwa chini mita 10,000

Simbu Pic1 Data Washindi wa mbio za uwanjani

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Mwanariadha Nyota wa Tanzania, Alfonce Felex Simbu amejikuta akipigwa bao na wanariadha chipukizi kutoka Arusha katika michuano ya mbio za uwanjani za mita 10,000.

Mashindano hayo ya Taifa ya mchezo wa riadha yanayoendelea mkoani Arusha, yameanza leo na yanatarajia kumaizika kesho jumamosi.

Simbu ambae amekuwa akikimbia mbio za barabarani za kilomita 21, ameshiriki mbio hizi za uwanjani kwa upande wa mita 10,000 akiwakilisha mkoa wa Singida na kuibuka nafasi ya tatu akimaliza kwa Dakika 31:03:19.

Nafasi ya kwanza katika mbio hizo zimeshikwa na wanariadha kutoka Arusha ambapo Faraja Damas ameongoza akimaliza kwa Dakika 31:02:19 akifuatiwa na Inyasi Sulle aliyetumia Dakika 31:02:60.

Akizungumzia ushindi wake Faraja amesema kuwa kwa Sasa anataka kufika mbali katika mchezo wa riadha hivyo mazoezi aliyoyaongeza ili kufikia malengo yake.

"Niwaombe viongozi wa Shirikisho la riadha Tanzania waongeze mashindano ya mbio za viwanjani ili kuwapa changamoto zaidi ya kufanya mazoezi na kufanya vema katika michuano ya kimataifa.

Kwa upande wake Simbu alisema kuwa amekuja katika mashindano hayo kuwakilisha mkoa wake alikozaliwa huku akisema kuwa hajali kupitwa na wanariadha chipukizi kwani riadha ni mchezo wa wote hivyo anafurahishwa na vijana wanaokuja kuwapa changamoto.

Chanzo: Mwanaspoti