Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbu aitosa Arusha, aibukia Singida

Iadha Pic Data Washiriki mchezo wa Riadha

Fri, 8 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Nyota wa mbio ndefu nchini, Alphonce Simbu ameibukia kwenye mashindano ya taifa ya riadha akiuwakilisha mkoa wa Singida alikozaliwa tofauti na wengi walivyotarajia angeuwakilisha mkoa wa Arusha anakoishi.

Simbu ni miongoni mwa nyota wanaochuana kwenye fainali ya mbio za mita 10000 inayoendelea kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Kwenye fainali hiyo, Simbu ameingoza hadi mzunguko wa tisa kwenye kundi la kwanza huku akipishana kwenye nafasi hiyo na Faraja Damas na Francis Fabiano.

Katibu wa riadha Arusha, Rogert Stephen amesema wameshangaa kumuona Simbu kwenye mashindano hayo kwani awali aliwambia hatoshiriki.

"Kwenda Singida ni uamuzi wa mchezaji mwenyewe, ingawa sisi alitueleza hatokimbia ndiyo sababu hatukumjumlisha kwenye timu ya Arusha,"amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz