Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbu afunguka sababu kushindwa Karatu

Simbu Felix Simbu Felix Simbu achemsha mbio za Kilomita 10

Fri, 24 Dec 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mwanariadha Alphonce Simbu amefichua kilichomkosesha ushindi kwenye mbio za kilomita 10 katika tamasha la Karatu lililofanyika kwenye viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu.

Simbu amemaliza wa saba akitumia dakika 32:56:32 akiachwa kwa sekunde 46 na bingwa, Faraja Lazaro aliyekimbia kwa dakika 32:00:42.

Simbu nyota wa mbio ndefu za barabarani za marathoni (kilomita 42) nchini alisema alizidiwa na wapinzani wake.

Hadi mzunguko wa mwisho, Simbu alikuwa sambamba na nyota wengine kwenye kundi lililokuwa mbele sanjari na Lazaro, Gabriel Geay na Fabian Sulle waliomaliza kwenye nafasi ya pili na ya tatu.

"Mimi ni mzoefu zaidi kwenye marathoni, hii ya kilomita 10 ina wenyewe, ndio sababu vijana walinipita," amesema Simbu.

Amesema ushindani aliokutana nao kwenye mbio hiyo unaashiri Tanzania ina wachezaji wazuri wa mbio za uwanjani za mita 5000 na 10,000 ambao wana uwezo wa kufanya vizuri kwenye michezo ya madola na mashindano ya dunia kama wataandaliwa mapema.

Geay alitumia dakika 32: 11:70 na Sulle alitumia dakika 32:18:35.

Wengine waliompiku Simbu ni Shingade Giniki na Inyasi Sulle ambao walimaliza wa nne na tano kwenye tamasha hilo lililodhamimiwa na Olympic Solidarity (OS) kupitia kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz