Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbu afanya maajabu China

Simba WA0003 Simbu afanya maajabu China

Sun, 26 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanariadha nguli wa Tanzania, Alphonce Simbu ametwaa nafasi ya pili kwenye mbio ndefu za Shanghai za nchini China (Shanghai Marathon 2023).

Muda aliotumia Simbu kumaliza mbio hizo ni saa 2:05:39, hivyo kujiweka kwenye mazingira mazuri kuelekea mashindano ya dunia ya France Olympic yatakayofanyika mwakani katika Jiji la Paris nchini Ufaransa, katika majira ya joto kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11.

Katika kuchagiza ushindi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amempongeza Simbu na Jackline Sakilu kwa kushika nafasi ya nne katika mashindano hayo.

“Wanariadha wetu hawa wamefanikiwa kufuzu kushiriki Mashindano ya Olympic 2024 na Wataungana na Wanariadha wengine Gabriel Gerald Geay na Magdalena Chripine ambao tayari walishafuzu kushiriki Olympic 2024,” amesema Msigwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live