Thu, 23 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania, Alphonce Simbu ameweka wazi kuwa tuzo ya Mwanamichezo bora wa kiume aliyoipata Machi 17, mwaka huu imempa deni la kuhakikisha anaongeza juhudi kuitangaza zaidi kimataifa.
Machi 17, mwaka huu Baraza la michezo Taifa (BMT), lilimtangaza Simbu kuwa Mwanamichezo bora wa kiume wa mwaka 2022 kupitia riadha.
Akizungumza nasi, Simbu alisema: “Nawashukuru wote ambao mmeendelea kunipa sapoti kubwa ya kuhakikisha nafika mahali nilipo, pia kwa tuzo ambayo nimeipata nadhani imenipa deni la kuhakikisha nafanya vizuri zaidi.”
Chanzo: www.tanzaniaweb.live