Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbu, Huche na Sulle washindwa kung’ara Qatar

78739 Simbu+pic

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Upepo mbaya umeendelea kwa timu za Tanzania, baada ya nyota Alphonce Simbu kushindwa kutetea medali yake ya shaba ya dunia usiku wa kuamkia leo Jumapili.

Mbali na Simbu, Agostino Sulle na Stephano Huche wameshindwa kumaliza mbio kwenye marathoni katika mashindano hayo yanayofungwa leo.

Waethiopia Lelisa Desisa aliyekimbia kwa saa 2:10:40 na Mosinet Geremew aliyekimbia kwa saa 2:10:44 ndiyo waliibuka vinara wa medali ya dhahabu na fedha huku Mkenya, Amos Kipruto akihitimisha tatu bora kwa saa 2:10:51.

Aliyekuwa bingwa mtetezi, Geoffrey Kirui raia wa Kenya amemaliza katika nafasi ya 14, nafasi moja zaidi ya Simbu ambaye alikuwa akitetea medali yake ya shaba.

Mtanzania huyo alimaliza katika nafasi ya 16 akitumia saa 2:13:57 akiachwa kwa dakika 3.17 na bingwa mpya wa msimu huu kutoka Ethiopia.

Wanariadha 19 waliochuana kutoka mataifa mbalimbali walishindwa kumaliza mbio wakiwamo Watanzania wawili, Sulle ambaye anashikilia rekodi ya taifa ya marathoni na Huche.

Pia Soma

Advertisement
 

Chanzo: mwananchi.co.tz