Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simbu, Failuna, Geay washinda kesi, kulipwa Sh450 milioni

Fidia Fidia Simbu, Failuna, Geay washinda kesi, kulipwa Sh450 milioni

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota watatu wa riadha nchini, Alphonce Simbu, Failuna Abdi na Gabriel Geay wameshinda kesi baada ya Mahakama ya Wilaya ya Arusha kuitaka Kampuni ya Multichoice kuwalipa fidia ya Sh450 milioni kwa kutumia picha za sura zao katika matangazo ya kibiashara bila ridhaa yao.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya kesi ya madai iliyofunguliwa na wanariadha hao ya kutumiwa kwa picha zao katika matangazo ya kibiashara bila ridhaa yao.

Pamoja na kiasi hicho cha fidia kila mmoja atalipwa Sh150 milioni, pia mahakama imeitaka Multichoice kuwalipa riba ya asilimia 25 ya kiasi hicho kuanzia tarehe waliyofungua kesi hiyo hadi tarehe ya hukumu.

Pia, imeamuriwa kuwalipa riba ya asilimia 10 ya kiasi hicho cha fidia, kuanzia tarehe ya hukumu hiyo yaani Novemba 30, 2022 hadi tarehe ya kumaliza malipo yote.

Hakimu Bittony Mwakisu alisema lazima ifahamike picha ya mwanamichezo ni rasilimali inayoonesha thamani ya kibiashara ambayo inaweza kumwingizia kipato na hakuna mtu anayeweza kunufaika nazo isivyo halali bila wanamichezo kuwa sehemu ya manufaa hayo.

Chanzo: Mwanaspoti