Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yawakwepa vigogo watatu Afrika

33864 Pic+mnyamaa%255D Tanzania Web Photo

Fri, 28 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

WAKATI zikiwa zimebaki saa chache kabla ya droo na upangaji wa ratiba ya Ligi ya Mabingwa na Kombe na Shirikisho Afrika, wawakilishi wa Tanzania Simba tayari wameshazikwepa timu tatu vigogo kutoka nchi tofauti Afrika. Timu ambazo Simba haitopangwa nazo kundi moja ni ASEC Mimosas ya Ivory Coast, CS Constantine ya Algeria na Orlamdo Pirates ya Afrika Kusini ambazo zote imewekwa nazo chungu kimoja wakisubili kupangiwa makundi na timu kutoka vyungu vingine. Katika tukio hilo ambalo litafanyika saa 12:00 jioni leo Ijumaa jijini Cairo Misri, Simba itawakilishwa na Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah 'Try Again' ambaye awali ndiye alikuwa Rais wa klabu hiyo. Hata hivyo, Simba licha ya kukwepa vigogo hivyo, bado ina kibarua cha kukutana na timu nyingine tatu miongoni mwa 12 ambazo zimewekwa katika vyungu tofauti.

Timu hizo ambazo Simba anaweza kupangwa nazo katika kundi moja ni Al Ahly (Misri), Eperance (Tunisia), TP Mazembe (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) na Wydad AC (Morocco) zilizo chungu cha kwanza, AS Vita Club (DRC), Club Africain (Tunisia), Horoya AC (Guinea) na Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)

Chungu cha nne kina timu za FC Platinum (Zimbabwe), Ismaily (Misri),JS Saoura (Algeria) na Lobi Stars (Nigeria)

S. Wawakilishi pekee kutoka Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika Simba wametinga katika hatua ya makundi msimu huu tangu walivyofanya hivyo mara ya mwisho 2003 na kutimiza jumla ya miaka 15.



Chanzo: mwananchi.co.tz