Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamtambulisha kocha mpya Mbelgiji Sven

88135 Pic+simba Simba yamtambulisha kocha mpya Mbelgiji Sven

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba imemtambulisha kocha wake mpya Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck leo Jumatano Desemba 11, 2019 akiwa na rekodi ya kufundisha timu mbili tu barani Afrika.

Vandenbroeck anachukua mikoba ya Patrick Aussems aliyetimuliwa hivi karibuni baada ya kuiongoza Simba kutwaa ubingwa Ligi Kuu pamoja na kufuzu kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Ujio wa kocha huyo mpya Simba umekuwa na siri kubwa tangu alipotua Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, ambapo alipokelewa na watu watatu wa timu hiyo na kumficha katika moja ya hoteli iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Waliokwenda kumpokea Vandenbroeck, alikuwa msaidizi wa idara ya habari na mawasiliano Rabi Hume, Dereva wa makocha wakuu wa Simba maarufu kama Michael Omog na mmoja wa watu wa karibu wa timu hiyo Matthew Shayo.

Baada ya kuwasili kwa Vandenbroeck hawakutaka kocha huyo atoke nje ya uwanja kwa kupitia mlango wa kawaida na kumpitisha nyuma kwa nyuma ili kukwepa waandishi walikuwa hapo.

Baada ya kumchukua kocha huyo walikwenda naye moja kwa moja katika hoteli ya Serena, ambapo walimficha hapo na kesho Alhamisi atakuwepo katika mazoezi ya Simba ambayo yatafanyika kuanzia saa 10:00 jioni.

Vandenbroeck, alianza kuwa kocha mkuu katika timu ya Niki Volou, iliyopo nchini Ugiriki mwaka 2014, akiwa kama kocha wa muda (Caretaker).

Baada ya hapo akawa kocha msaidizi wa timu ya Oud-Heverlee Leuven na timu ya taifa ya Cameroon, ambayo alikuwa akifanya kazi ya usaidizi chini ya kocha mkuu Hugo Broos, ambapo mwaka 2017, walichukua ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika.

Vandenbroeck, baada ya hapo alikwenda kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zambia Julai 2018, baada ya kuingoza timu hiyo Februari 2019, Shirikisho la soka la Zambia, walitangaza kutokuongeza mkataba wa kocha huyo aliokuwa na timu hiyo kwa mwaka mmoja tu.

Zambia waliamua kuvunja mkataba wa Vandenbroeck, Machi 2019, kutokana na kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika zilizofanyika nchini Misri.

ALIVYOKUWA MCHEZAJI

Sven Ludwig Vandenbroeck, amezaliwa Septemba 22, mwaka 1979, mpaka sasa ametimiza miaka 40, amezaliwa katika Mji wa Vilvoorde, nchini Belgium.

Kabla ya kuwa kocha alianza kucheza mpira kama kiungo mkabaji mwaka 1996–2000, katika timu ya Mechelen, baada ya hapo mwaka 2000–04, alikwenda kujiunga na timu ya Roda JC ambapo alicheza mechi 55 na kufunga bao moja tu.

Mwaka 2004–05, Vandenbroeck alijiunga na De Graafschap ambapo napo alicheza mechi 19, bila kufunga bao kama ambavyo alikwenda timu ya Akratitos mwaka 2005, akacheza mechi moja bila kufunga.

Vandenbroeck mwaka 2006–07, alijiunga na Lierse ambapo napo alicheza mechi 23, bila kufunga bao lolote wakati mwaka 2007–08, alijiunga na Vise na baada ya msimu kumalizika mwak 2009, alijiunga na Løv-Ham ambapo alicheza michezo mitatu tu bila kufunga bao.

Chanzo: mwananchi.co.tz