Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamrudisha Dida Yanga

20120 Pic+dida TanzaniaWeb

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kipa wa Simba, Deogratius Munishi 'Dida' ameonyesha kuwa ni mwanamichezo wa kweli baada ya kwenda kuwapa  'hi' benchi la ufundi la Yanga na wachezaji wenzake kabla ya mechi kuanza.

Dida mchezaji wa zamani wa Yanga, kabla ya kuanza kwa mchezo huo, alikwenda moja kwa moja mahali lilipo benchi la ufundi la vijana hao wa Jangwani na kuwasalimia wote kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho.

Na wakati anawasalimia hivyo, Mrundi Amissi Tambwe ndiye alitumia muda mrefu hadi kukumbatiana.

Hali ambayo imeonyesha kuwa, huenda jamaa hao walikuwa karibu.

Katika hali ya kawaida tukio kama hilo kufanyika ni la kipekee kwani wachezaji na mashabiki huwa katika 'tensheni' kutokana na ushindani wao.

Na baada ya tukio hilo, Dida alirudi kwenye benchi la timu yake ya Simba akatulia kusubiri mchezo uanze.

Awali, Dida aliichezea Yanga kwa mafanikio kabla ya kwenda nchini Afrika Kusini.

Chanzo: mwananchi.co.tz