Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yamlilia shabiki wao Ruge Mutahaba

44112 Pic+simba Simba yamlilia shabiki wao Ruge Mutahaba

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Klabu ya soka ya Simba imeshitushwa na msiba wa Mkurugebzi wa vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba uliotokea jana nchini Afrika Kusini.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara imesema Ruge ameacha pengo siyo tu kwa CMG bali kwa jamii ya Watanzania.

Taarifa hiyo ilisema Ruge alikuwa mwanachama na shabiki wa Simba.

"Kwenye uhai wake alijihusisha kwenye harakati nyingi za maendeleo ya vijana na kuwainua walio wengi hapa nchini, pengo lake ni kubwa," ilisema sehemu ya taarifa hiyo na kufafanua.

"Simba inawapa pole familia, CMG, pamoja na wote walioguswa na msiba huu mzito uliogusa watu wengi nchini," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz