Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaisubiri Nkana

31656 PIC+NKANA TanzaniaWeb

Fri, 14 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Daktari wa Simba Yassin Gembe alisema wachezaji wote wa wapo kamili na hakuna mwenye majeruhi.

Gembe alisema tangu wamefika hapa Kitwe Zambia wakiwa name kikosi cha wachezaji 20 wote wamefanya mazoezi na hakuna aliyekuwa na shida yoyote.

"Kama majeruhi labda apatikane katika mazoezi ya jioni ya leo lakini mpaka Sawa hakuna aliyekuwa na majeraha yoyote, " alisema.

"Kama unavyowaona wachezaji wote wapo katika morali ya hali ya juu na matumaini yetu makubwa ni kupata ushindi katika mechi ya kesho, " alisema.

"Kwangu ni kuangalia wachezaji wote wanakuwa salama kiafya kabla ya mechi na muda wote wanapokuwa kambini, " alisema Gembe.

Simba watafanya mazoezi ya mwisho leo jioni katika uwanja wa mechi.



Chanzo: mwananchi.co.tz