Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaipiga 'kijembe' Yanga ikiteseka njiani

69679 Pic+manara.png Simba yaipiga 'kijembe' Yanga ikiteseka njiani

Fri, 12 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UTANI wa jadi wachukua nafasi, ndivyo unavyoweza kusema baada ya Simba 'kuwapiga dongo' watani zao baada picha kusambaa ikionyesha basi la Yanga lililobeba kikosi cha timu hiyo kuharibika wakiwa njiani kuelekea Shinyanga.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema timu inayofanya mabadiliko inatakiwa ijiwekee 'ukubwa' wa timu yao na kutokubali kufanya mambo ya kushusha taswira ya klabu.

"Timu inajiita kubwa inafanya mabadiliko halafu wachezaji wanasafiri kwa basi kwa umbali mrefu tena kwa basi lililochoka, wanafika sehemu linaharibika, wanafika mbele wanasimama kununua mahindi au mayai, haiwezekani," alisema Manara.

Kiongozi huyo alisema Yanga wanapaswa kuiga kutoka kwao (Simba), ambao hawakubali timu isafiri kwa njia ya barabara katika umbali wa zaidi ya kilometa 300.

"Simba inaonyesha kwa vitendo ukubwa wa timu yao, haikubali wachezaji wasafiri zaidi ya kilometa 300 kwa kutumia basi, zaidi ya kilometa hizo ni ndege tu, hiyo ndio maana ya timu kubwa," Manara alisema.

Manara alisema pia kitendo cha mchezaji wa Yanga (David Molinga), kupiga simu katika kituo cha redio na kulalamika moja kwa moja, hali hiyo inaonyesha timu hiyo ina udhaifu au ni yenye hadhi ya chini.

"Simba huwezi kukuta Chama (Clatous), anapiga simu redioni kulalamika, mambo ya timu yanamalizwa ndani ya timu kwa taratibu za timu, hiyo ndio maana ya timu kubwa, timu kubwa ni vitendo sio porojo," aliongeza Manara.

Kauli hiyo ya Manara imekuja siku moja baada ya Molinga kulalamika kwenye kituo kimoja cha radio alikataa kusafiri na kikosi cha Yanga kuelekea Shinyanga kwa sababu hakuwa kwenye mipango ya kocha, jambo ambalo lilikanushwa na viongozi wa klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live