Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yainyima 'raha' Namungo

SIMBAAA Simba yainyima 'raha' Namungo

Mon, 6 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Namungo FC, Mrundi, Thiery Hitimana, amesema ana 'kazi kubwa' kuhakikisha nyota wa Simba hawafurukuti katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaowakutanisha keshokutwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, mkoani Lindi.

Namungo FC itakuwa wenyeji wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba katika mchezo wa raundi ya 33 na baada ya mechi hiyo, Wekundu wa Msimbazi watakabidhiwa kombe lao la ubingwa.

Hitimana aliliambia gazeti hili ana 'kibarua kinene' kuhakikisha anapanga kikosi imara ili kukabiliana na wachezaji wa Simba, ambao wanauzoefu na wana kiu ya kuendelea kushinda.

Kocha huyo alisema aliiangalia vema mechi kati ya Simba na Azam, na ameahidi kuwakabili nyota wapinzani wao kwa namna mpya.

"Niliuangalia mchezo wa robo fainali ya FA, Simba na Azam, kwa kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wa kikosi cha Simba, ninaamini nitakuwa na mechi ngumu, nimecheza na Simba mzungumzo wa kwanza, sikuwa na presha kama ilivyokuwa sasa, ukisema umkabe Chama (Clatous), basi kuna yule wa Msumbiji (Luis Miquissone) ni hatari, Kagere (Meddie), ninamfahamu, hana mchezo," Hitimana alisema.

Aliongeza amewataka wachezaji wake kutulia na kufuata maelekezo, kwa sababu mpira ni mchezo wa makosa na endapo wapinzani wao watateleza, watatumia vema nafasi hiyo.

"Nakiandaa kukabiliana na mchezaji yoyote, siwezi kutoa maelekezo ya kumzuia Chama au Kahata (Francis), wakati anakuja kucheza Deo Kanda au Miraji Athuman," aliongeza kocha huyo.

Hitimana alisema mbali na Simba kuwa vizuri pia kitendo cha kukabidhiwa kombe mbele yao kinawapa wakati mgumu katika kusaka ushindi kwenye mchezo huo.

"Suala la kukabidhiwa kombe kwetu wametupa mtihani mkubwa, kwa sababu hawatahitaji kuona wanapokea kombe tena baada ya kufungwa," Hitimana aliongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live