Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaichapa Singida United yapaa kileleni na rekodi yakutisha

81952 Pic+miraj Simba yaichapa Singida United yapaa kileleni na rekodi yakutisha

Mon, 28 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba imeendeleza rekodi yake ya ushindi kwa asilimia 100 kwa kuichapa Singida United kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mshambuliaji Miraji Athumani alifungia Simba bao pekee katika dakika 41 kipindi cha kwanza na kuwahakikishia mabingwa hao watetezi ushindi wa sita mfululizo katika Ligi Kuu.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 18, katika michezo sita na kuwa timu pekee ambayo haijafungwa hadi sasa katika Ligi Kuu Bara baada ya Azam leo kufungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting.

Katika mchezo huo, Simba ilitawala na kulishambulia lango la Singida United kikwazo kikubwa kwao alikuwa kipa Mkumbo Msafiri aliyefanya kazi ya ziada kuokoa hatari nyingi golini kwake.

Mshambuliaji Miraji Athumani alifunga bao pekee kwa Simba katika dakika ya 41, alipiga shuti kali lililomshinda kipa Singida United, Mkumbo Msafiri.

Hilo ni bao la nne kwa Miraji msimu huu akiendeleza harakati zake za kumkimbiza Meddie Kagere mwenye mabao saba katika kikosi cha Simba.

Pia Soma

Advertisement
Simba imefunga mabao 12, yamefungwa na wachezaji watatu ambao ni Kagere, Miraji wanaocheza katika safu ya ushambuliaji pamoja na nahodha msaidizi Mohammed Hussein 'Tshabalala'.

Athumani alisajiliwa na Simba msimu huu akitokea Lipuli huenda hakupewa nafasi kubwa katika orodha ya nyota ambao walitegemewa kufanya vizuri kama Ibrahim Ajibu, Mbrazil Wilker Da Silva, Francis Kahata na wengine.

Kutokupewa nafasi kwa Athumani pengine kulitokana na udogo wa jina lake na timu aliyotoka, lakini mpaka sasa mambo yamekuwa tofauti kutokana na moto aliyo uwasha.

Katika michezo sita ambayo Simba wamecheza Athumani amefunga timu nne ambazo ni JKT Tanzania, Mtibwa Sugar, Biashara United na Singida United, timu ambazo hajazifunga ni Azam ambayo hakucheza pamoja na Kagera Sugar aliingia kipindi cha pili na kusababisha penati ambayo Kagere bao.

Mchezo huo ulikuwa unachezeshwa na mwamuzi Ahmada Simba wa Kagera akisaidiana na Makame Mdogo wa Shinyanga na Robert Mhemeja wa Arusha na Emmanuel Mwandembwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz