Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yagomea waamuzi wa CAF

51252 SIMBA+PIIC

Wed, 10 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Klabu ya Simba imeandika barua kwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupinga mabadiliko ya waamuzi katika mechi yao ya Jumamosi dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo.

Akizungumza jana, Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori alisema wameandika barua ya kulalamika kutoridhishwa na mabadiliko ya waamuzi zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mchezo.

Magori alisema kitendo hicho kimewapa hofu kutokana na ukubwa wa mchezo huo na ule wa awali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambao timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.

Alisema wanafahamu miongoni mwa wamiliki wa TP Mazembe Moise Katumbi anafanya shughuli zake Zambia ambapo waamuzi hao wapya wanatoka.

“Kwa hali ya kawaida ukaribu wa Ndola, mji anaotoka mwamuzi mpya, Janny Sikazwe anatumia saa mbili tu kwa gari mpaka Lubumbashi ambapo tutacheza mechi ya marudiano.

“Tumefikisha malalamiko yetu CAF ili kushughulikia jambo hili mapema,” alisema Magori.

Awali, waamuzi waliopangwa kuchezesha mechi ya marudiano ni mwamuzi wa kati, Bamlak Tessema (Eithiopia), mwamuzi msaidizi, Temesgin Samuel (Eithiopia), Gilbert Kipkoech (Kenya), mwamuzi wa akiba Peter Waweru akitokea Kenya.

Kwa mujibu wa barua iliyotoka CAF kwenda Simba Aprili 7, ilisema waamuzi hao walibadilishwa kwa sababu za kiufundi ambazo hawakuzitaja.

Waamuzi wapya ni mwamuzi wa kati Sikazwe anayetokea Zambia, mwamuzi msaidizi Berhe Tesfagiorgis (Eritrea) na Romeo Kasengele (Zambia).

Mwamuzi wa akiba Audrick Nkole (Zambia), Aimable Habimana wa Burundi kamishna na Salah Ahmed kutoka Sudan atakuwa msimamizi wa waamuzi.



Chanzo: mwananchi.co.tz