Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafyeka kiporo kingine Taifa ikiifunga Singida mabao 3-0

Sat, 29 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Timu ya Simba imeibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Taifa jijijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yaliwekwa wavuni na John Bocco, Shiza Kichuya (2) na kuifanya timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi kufikisha alama 33 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Ni umakini tu wa pasi za mwisho kwa nyota wa Simba zilizowafanya wapate mabao ya mapema. Kipindi cha kwanza eneo la kiungo wapo Jonas Mkude, Cleutous Chama na James Kotei walijitahidi kumiliki mipira vyema tatizo ilikuwa pasi za mwisho zinakuwa hazifiki ipasavyo. Umakini wa winga Shiza Kichuya dakika ya 17, alimtazama John Bocco na kumpa pasi aliyoitendea haki kwa kuusukumiza mpira nyavuni ambako alikaa mlinda mlango wa Singida United, Ally Mustapha 'Bartez'. Simba walitumia kupita upande wa mabeki wa kulia wa Singida ni umakini mdogo wa Nickolas Gyan ambaye anachelewa kupanda ili kuwasaidia mastraika wa kati Bocco na Okwi kwa kuwa anacheza kama beki wa pembeni kucheza kama mawinga. Kwa upande wa Singida wanapopoteza mipira wanawahi kurudi kwenye nafasi zao na wamekuwa na mashambulizi ya hapa na pale ingawa washambuliaji wao hawakai na mpira miguuni.



Chanzo: mwananchi.co.tz