Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafunga TV kwa Mkapa

Tv Pic Data Simba yafunga TV kwa Mkapa

Sun, 19 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

TUKO ‘live’! Ndio tambo za mashabiki wa klabu ya Simba waliopo ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa muda huu kwenye Simba Day kutokana na kufungiwa Runinga (TV) mbili ambazo zinaonesha mubashara kila tukio linaloendelea.

Simba leo kwenye tamasha la Simba Day, imefunga TV hizo mbili katika maeneo mawili tofauti ambapo moja ipo kulia na nyingine kushoto nyuma ya goli moja la uwanja huo.

TV hizo zinaonesha kila tukio linaloendelea Uwanjani hapa na mashabiki wanaonekana kufurahia zaidi kwani wanajiona namna wanavyoshangilia huku wakitamba kuwa haijawahi kutokea.

John Mnyama na Aisha Dida ni miongoni mwa mashabiki walioonesha kufurahia zaidi siku ya leo sambamba na TV hizo.

“Tuko live, Sisi ndio Simba na waanzilishi wa kila kitu kizuri kwenye michezo nchi hii. Kama unavyoona leo tumeanza na TV mbili kufika jioni tutakuwa na sapraizi kibao,” amesema Aisha.

Naye John amesema; Hii haijawahi kutokea, tunaanzisha sisi na wengine wanafuata na leo tunaujaza uwanja kabla ya saa tisa,” amesema.

Tayari mashabiki wa Simba wapo kwa wingi ndani ya uwanja huku wengine wakiwa nje kwenye mageti wakisubiri kuingia ndani kuendelea na Tamasha la Simba Day.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz