Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yafanya kweli Ligi ya Mabingwa Afrika, yaiondoa Nkana

33114 Ushindi+pic Kikosi cha Simba

Sun, 23 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Timu ya Simba imetinga hatua ya makundi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Nkana mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Nkana imetolewa kwa jumla ya mabao ya mabao 4-3 huku ikiangukia kwenye Kombe la Shirikisho.

Licha ya kufunga bao lililoifanya Simba kuwa mbele ya Nkana Red Devels  kipindi cha kwanza kwa mabao 2-1, mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere alipiga pasi nne. Kagere ambaye mara kadhaa alikuwa akipoteza mipira ameifungia Simba bao hilo mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kuanzwa kwa kona fupi. Simba ilianza kutanguliwa kwenye kipindi hicho cha kwanza kabla ya muda mchache baadaye kusawazisha kwa shuti kali la kiungo,  Jonas Mkude. Ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza aliyrpiga pasi nyingi kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba ni Mganda Emmanuel Okwi mwenye pasi 11, John Bocco alipiga sita zilizowafikia walengwa. Aliyepiga pasi chache zaidi kwenye kikosi cha Simba ni mlinda lango wao,  Aishi Manula ambaye ameruhusu nyavu zake kuguswa mara moja.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz