Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yachezea kichapo mbele ya Rais Magufuli

98389 Magufuli+pic Simba yachezea kichapo mbele ya Rais Magufuli

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli kwa mara ya pili anaishuhudia Simba ikifungwa bao 1-0 na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Rais Magufuli ni shabiki wa Simba aliingia uwanjani hapo saa 10:40 jioni ikiwa ni muda mchache baada ya Rais wa CAF, Ahmed Ahmed kuingia uwanjani hapo.

Rais Magufuli alikuwa amevaa jezi yake ambayo nusu ilikuwa na rangi ya Yanga na upande mwingine rangi nyekundu huku akiwa amevaa kofia yenye rangi ya bendera ya Tanzania.

Leo Rais Magufuli akiwa amekaa jukwaani na mgeni wake rais wa CAF, Ahmed alishuhudia Simba ikipokea kipigo kingine cha bao 1-0 kutoka kwa watani zao wa jadi.

Mshambuliaji Bernard Morrison alifunga bao pekee la Yanga kwa mpira wa adhabu katika dakika 44 na kuhamsha shangwe kwa mashabiki uwanjani hapo.

Bao hilo lilimfanya Rais Magufuli kufurahi na kuwapungia mashabiki wa Yanga waliolipuka kwa shangwe kubwa baada ya bao hilo.

Pia Soma

Advertisement

Mara ya mwisho Rais Magufuli alipokuwa uwanjani hapo alishuhudia Simba ikipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar msimu wa 2017/18.

Baada ya mchezo huo Rais Magufuli wakati akiikabidhi Simba ubingwa msimu 2017/18, alisema Kagera Sugar ikitoboa tundu na kuongeza kusema kwa mpira huu unaocheza hamuwezi kuchukua ubingwa wa Afrika.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz