Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaanza mkakati kimataifa

E98df8767b4fcde93f8dbe4c6a7ae040.png Simba yaanza mkakati kimataifa

Wed, 5 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

BAADA ya mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba kutimiza malengo ya kuchukua mataji matatu msimu huu, mkakati ujao wanatazama kutengeneza historia ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

Mataji iliyochukua Simba ni ngao ya jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ikiwa ni timu pekee iliyoshinda mataji mengi msimu huu.

Akizungumza baada ya kutua Dar es Salaam juzi wakitokea Rukwa kwenye fainali ya ASFC, Kocha Sven Vandebroeck, alisema kitu wanachotazama ni michuano ya kimataifa na lengo la kwanza ni kuhakikisha wanavuka hatua ya makundi.

“Lengo letu la kwanza tunaangalia michuano ya kimataifa, namna gani ya kujenga timu ya kufikia hatua ya makundi na kuivuka,”alisema.

Alisema kama watavuka zaidi ya hatua hiyo itakuwa jambo jema lakini muhimu kwanza ni hilo. Simba na Namungo ndio timu zitakazowakilisha nchi kimataifa mwakani, hivyo zinatarajiwa kuanza maandalizi ya usajili mpya kujenga vikosi vyao.

Aidha, Simba wanataka kufuta kilio kilichowakuta msimu huu katika michuano hiyo baada ya kutolewa mapema ingawa Vandebroeck alisema muda unahitajika kukua na kuwa bora.

Msimu wa mwaka juzi, Simba iliishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuweka historia mpya ya michuano hiyo baada ya miaka kadhaa kupita.

Msemaji wa Simba, Haji Manara alisema ubora wa kikosi chao kwa sasa unataka kushindana na timu bora Afrika kwa kusajili wachezaji wenye hadhi ya kupambana kimataifa.

Chanzo: habarileo.co.tz