Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Simba yaaga kwa kishindo

5213d841366793178065e25cef4bc854.jpeg Simba yaaga kwa kishindo

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SIMBA imemaliza michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara katika Uwanja wa Taifa na imetoa zawadi ya ubingwa kwa mashabiki wao wa Dar es Salaam kwa kuifunga Alliance FC kwa mabao 5-1.

Kabla ya mchezo huo, mashabiki walipata wasaa wa kupiga picha na kombe la ubingwa wa ligi ambalo Simba walikabidhiwa katika mchezo dhidi ya Namungo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa Lindi, Julai 8.

Na baada ya mchezo, wachezaji na benchi la ufundi walizunguka uwanjani wakiwa na kombe lao kama ishara ya kuwashukuru kwa sapoti yao kwani michezo miwili iliyobaki watacheza ugenini.

Katika mchezo wa jana bao la kwanza la Simba lilifungwa na Meddie Kagere kwa penalti dakika ya 23 lakini dakika ya 39 Kigi Makassy aliisawazishia Alliance na Medie Kagere akaongeza bao la pili dakika ya 44 na kwenda mapumziko wakiwa mbele Kipindi cha pili Simba ilianza mchezo kwa kasi na dakika ya 64, Luis Miquissone analifunga bao la tatu ambalo unaweza kuliita bao bora la msimu kutokana na ufundi na juhudi binafsi alizotumia hadi kufunga.

Dakika ya 75 Deo Kanda alifunga bao la nne na dakika ya 86, Said Ndemla alifunga karamu ya mabao kwa kufunga bao la tano Kwa matokeo hayo msimu huu, Alliance FC imefungwa na Simba jumla ya mabao 9-2 baada ya mchezo wa mzunguko wa kwanza kufungwa mabao 4-1 katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kwa sasa Meddie Kagere amefikisha mabao 22 msimu huu huku Simba ikifikisha pointi 84, inafuatiwa na Yanga inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 68, Azam FC inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66 na Namungo FC nafasi ya nne ikiwa na pointi 64 na wote wamecheza michezo 36.

Alliance FC inashika nafasi ya 17 ikiwa na pointi 41 sawa na Mtibwa Sugar, Lipuli na Mwadui zote zipo kwenye mstari wa kushuka daraja au kucheza mechi za mtoano. Katika mchezo mwingine Lipuli ilitoka sare ya 1-1 na Azam FC na JKT Tanzania ililazimishwa sare ya 1-1 na Mbao FC.

Chanzo: habarileo.co.tz